Kituo cha redio cha huko Houston, Marekani kimewafukuza wafanyakazi wake wote 47 na kuamua kucheza nyimbo za Beyonce 24/7.
News92 ilikuwa ni redio kwaajili ya habari peke yake. Uamuzi wa kubadilisha malengo ya kituo hicho umetokana na kituo hicho kukosa wasikilizaji. Uongozi unaamini kuwa kwa kupiga nyimbo za Beyonce wasikilizaji watavutiwa na kuiokoa redio hiyo iliyopo kwenye mawe.
Kituo hicho kitaendelea kucheza nyimbo za Beyonce kwa saa 24 hadi pale itakapotangaza muelekeo wake mpya.