Lorraine Clement akimshukuru Mungu, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA), akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.
Julius Nyerere (JNIA), akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji.
Lorraine kiwa na familia yake na mama yake (kulia).
Na Andrerw Chale
MWANADADA Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok, Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
Akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
“Pongezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha, Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Katika mapokezi hayo, Lorraine alilakiwa pia na wazazi wake pamoja na mtendaji Mkuu wa Redline Communication, Abubakar Faraji ‘Abu’ na wadau wengine walijitokeza uwanjani hapo.
Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Lorraine, Paula David aliwashukuru watanzania kwa kumpigia kura mwanae na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Hii ni kwa mara kwanza, mtanzania huyo anashiriki shindano hilo ambalo kwa hapa nchini linaendeshwa na kampuni ya Redline Communication Ltd, ambapo mshiriki wake huitwa ‘Miss Grand Tanzania’, kwa mwaka huu, Lorraine alikuwa ni mshindi wa pili kwenye shindano la Tanzania Top Models 2013.
Aidha, Katika shindano hilo, mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi ya Cuba, ndiye aliyetwaa taji hilo kwa mwaka huu. Wengine ni Miss Ethiopia, Hiwot Mamo na Miss Canada, Kathryn Kohut.
Shindano hilo la Miss Grand International, kwa sasa ni msimu wa pili likifanyika nchini Thailand, tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa mwaka huu, ameweza kunyakua kitita taslimu cha dola za kimarekani 40,000, pamoja na thamani za ndani.