Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana
na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam jana, ilisema
tayari Rais Kikwete amepokea Ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kwa mujibu wa
taarifa hiyo, ilisema Rais Kikwete pia amepokea nyaraka na ushauri uliotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusu sakata hilo.
taarifa hiyo, ilisema Rais Kikwete pia amepokea nyaraka na ushauri uliotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusu sakata hilo.
“Rais Kikwete ameanza kupitia na kusoma
nyaraka hizo, wiki ijayo atatoa maamuzi katika mambo yanayomhusu yeye na
yale yanayoihusu Serikali, atayatolea maagizo na maelekezo ya namna ya
kuyashughulikia.
“Baada ya kurudi nchini akitokea
Marekani ambako alifanyiwa upasuaji wa tezi dume, Rais alianza kazi
Desemba 8 mwaka huu,” ilifafanua taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, Rais
Kikwete ameelekeza Ripoti ya CAG iwekwe hadharani ili umma uweze kuisoma
na kujua nini kimesemwa, kupendekezwa na CAG.
Pia ameagiza ripoti hiyo itangazwe katika magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya kijamii.
Akutana na viongozi wa dini
No comments:
Post a Comment