Juma Nature amesema tabia ya uongo kwa wanawake wengi inamfanya asifikirie kuoa awe mgumu kuoa.
Nature ambaye ni baba wa mtoto mmoja aitwaye Furaha, ameiambia Bongo5
kuwa anashidwa kufanya uchaguzi sahihi wa mwanamke kutokana na wanawake
kuwa matapeli.
“Suala la kuoa ni suala la kitaifa, siku mimi nikioa hata rais atajua
Juma Nature anaoa, nikiwa tayari hata rais atafahamu kwamba mchizi
anachukua jiko.”
“Mimi kuoa bado sana, nashukuru mungu sasa hivi nina mtoto ‘Furaha’
anasoma vizuri anaongea kiingereza mpaka kichina. Tatizo linalonifanya
nisioe na ni nisifirie kuoa ni watu hawakai ndani, watu waongo sana sasa
hivi, sasa hivi wanawake wengi sana waongo waongo, unaweza ukasema
nifanye naye maisha kumbe ndo cheche huyo. Sasa utaoa vipi wakati kila
unayekutana naye unamuona kabisa huyu ni tapeli.”
Pia Nature amewaka watanzania kuendelea kusupport wimbo wake mpya unaoitwa Komaa uliotoka sambamba na video.
No comments:
Post a Comment