Nyota huyo aka Mr. Kukere ambaye mwaka jana pia alikuja Tanzania na kutumbuiza katika tamasha la Fiesta Dar es salaam, ameachia single mpya iitwayo ‘Story story’ Feat. Oritsefemi.
Hivi karibuni Iyanya pia ameshoot video ya single yake nyingine ambayo audio yake ilishatoka,‘Mr Oreo’.
Uchukuaji wa picha za video hiyo umefanyika wakati wa tour yake ya Marekani na kuongozwa na director aitwaye The Mega Boi.
Tazama picha za behind the scene:
MZIKI NI BURUDANI AMBAYO HUMFURAHISHA KILA MWANADAMU KATIKA KATIKA MAISHA. NA HATA WENGINE HUWAPUNGUZI MZIGO WA MAWAZO WAKATI MSONGO WA MAWAZO YAHUSUYO MAISHA
WASANII 12 WA BONGOFLEVA TANZANIA WENYE NGUVU ZAIDI MWAKA 2014
Wana mashabiki wengi, miongoni mwao tayari ni mamilionea (wa shilingi), wapo wenye mijengo, magari ya kifahari, miradi ya biashara, makampuni, endorsements na vitu vingine. Hawa ndio wasanii 12 wa Tanzania wenye nguvu zaidi mwaka 2014.
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz ndiye msanii anayeandikwa zaidi kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki kwa sasa. Hadi sasa Diamond amefikia hatua ambayo haijawahi kufikiwa na msanii yeyote wa Tanzania. Ndiye msanii mwenye show nyingi zaidi kwa sasa.
Kimataifa 2014 umekuwa wa mafanikio zaidi kwake kuanzia kutajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo za MTV MAMA, BET Awards, kushiriki kwenye wimbo uliokutanisha mastaa takriban 20 wa kampeni ya ‘Do Agric’ ‘Cocoa na Chocolate, pamoja na wimbo ‘Africa Rising’ uliomkutanisha na wasanii kama Mi Casa Music, Davido, Sarkodie na Tiwa Savage.
Diamond akihojiwa na Karrueche Tran kwenye red carpet ya BET Awards, June 29, 2014
Pia pamoja na kufanya wimbo na Davido, Diamond ameshafanya collabo na wasanii wengine wa Nigeria wakiwemo Iyanya, Waje na Dr Sid pia hivi karibuni ameshirikishwa na kundi la Afrika Kusini, Mafikizolo.
Wema akiwa pembeni kumsupport Diamond
Diamond na Wema kwenye red carpet ya MTV MAMA 2014, Durban, SA
Pamoja na kukosa tuzo za kimataifa alizotajwa kuwania, staa huyo mwaka huu alivunja rekodi kwa kuchukua tuzo zote saba alizotajwa kwenye KTMA na pia kushinda tuzo za watu zilizotolewa June 27.
Akiwa na video mbili mpya kibindoni, moja ya wimbo aliofanya na Iyanya na ile ya wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’, Diamond ana uhakika wa kuendelea kuutawala mwaka 2014.
Lady Jaydee
Lady Jaydee pamoja na Machozi Band akitumbuiza
Judith Mbibo aka Lady Jaydee ndiye msanii wa kwanza wa Tanzania kufikisha likes 300,000 kwenye mtandao wa Facebook huku sasa idadi ikiwa ni zaidi ya 329,000. Tangia June mwaka jana alipofanya show yake ya miaka 13 ya muziki wake na kuijaza Nyumba Lounge watu wasipate pa kukanyaga, Lady Jaydee haoneshi dalili za kusimama. Baada tu ya kutoka kwenye Coke Studio Africa, Jaydee alishiriki kwenye wimbo maalum kwaajili ya kombe la dunia wa Coca Cola, ‘The World is Ours’. Pamoja na show zisizo katika, biashara yake kuu ya mgahawa imeendelea kufanikiwa.
Kwa mujibu wa meneja wake, Gadner G Habash ambaye pia ni mumewe pamoja na kuwa na biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee anatarajia kuongeza zaidi miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali mchanga anayejifunza zaidi na angependa kufanya biashara nyingi lakini muda ni mdogo. Isipokuwa kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine kuongeza kama biashara. Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini mwenyezi Mungu akijaalia heri na afya mwaka huu kuna biashara nyingine Jaydee ataitambulisha, ukiacha Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner aliiambia Bongo5 kwenye mahojiano maalum.
Mwaka huu Jide alipata pia endorsement kutoka kwenye kampuni ya vipodozi ya Sweden Oriflame Cosmetics na kuungana na wanawake wengine watatu maarufu wa Afrika Mashariki kuwa mabalozi wa bidhaa zao katika nchi zao. “Lady Jaydee, Juliana and Jamila have been named because their style and approach to beauty is the ideal representation for the Oriflame brand. They are strong and talented women who many people across East Africa readily identify with,”alisema mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Afrika Mashariki Mr. Klas Kronaas wakati akiwatangaza.
June 28, Lady Jaydee alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tukio la Masaku Rugby 7s After Party lililofanyika huko Machakos Kenya. Takriban watu 40,000 walihudhuria kwenye show hiyo iliyodhaminiwa na Tusker Lager. Wasanii wengine walitumbuiza ni pamoja na Jua Cali, Radio n Weasel, Wyre, Kidum, Keni wa Maria.
Kingine ni kubwa ni kuwa Lady Jaydee ataungana na Ali Kiba kutoka Tanzania kupanda jukwaa moja na Nicki Minaj, J Cole na wasanii wengine wa Marekani na Afrika kwenye tamasha la TribeOne Dinokeng litakalofanyika September mwaka huu nchini Afrika Kusini.
AY