button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

LIFE

"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.


Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye
mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga lakini aliipinga sana.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulishanyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia baruahii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyikanakufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie vibayamaana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako
AMENITENDA HIVI!!!
LIKE & SHARE







Siku ya Vijana Duniani: Tusipokabiliana na ukosefu wa ajira na kupewa nguvu ya maamuzi, hatutaweza


group of african american college students
Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka, kuwa ‘Siku ya Vijana Duniani’ ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema ‘Vijana na Afya ya Akili’.Kwa mujibu wa andiko kutoka Umoja wa Mataifa, asilimia 20 ya vijana duniani kote hupata tatizo linalohusiana na afya ya akili kila mwaka. Hatari zaidi hutokea katika kipindi cha kuhama kutoka utoto kuingia utu uzima.
Kutengwa pamoja na aibu mara nyingi huongeza zaidi tatizo kwakuwa vijana wengine hushindwa kutafuta msaada wanaouhitaji. Hivyo mwaka 2014, Umoja wa Mataifa umeazimia kuitumia siku hii kukuza uelewa kuhusu afya ya akili kwa vijana.
“Wakati tunaadhimisha Siku ya Vijana Duniani 2014, tuwawezeshe vijana wenye matatizo ya afya ya akili kubaini umuhimu wao, na tuoneshe kuwa afya ya akili inatuhusu sote,” amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Maitafa, Ban Ki Moon kwenye maelezo yake.
Miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia tatizo la afya ya akili ni umaskini unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa ajira. Asimilia kubwa ya vijana walio chini ya miaka 25 au wale wanaohitimu masomo yao nchini hawana ajira.
Wanachuo wengi wameendelea kuzunguka huku na kule kuomba kazi bila mafanikio. Wengi wamekaa zaidi ya miaka mitatu nyumbani tangu wamalize masomo yao bila kuwa na ajira inayowaingizia kipato.
Na pia wachache wanaopata kazi, wamekuwa wakilipwa ujira mdogo na hivyo kuendelea kuishi maisha magumu. Ukosefu wa ajira na kukosa fedha za kujikimu, umewafanya vijana wengi kuwa na msongo wa mawazo, tatizo kubwa linalohusiana na afya ya akili.
Tatizo ni kubwa zaidi pale ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa wastani soko la ajira nchini lina uwezo wa kuzalisha ajira zipatazo 300,000 kwa mwaka katika sekta rasmi ukilinganisha na wastani wa wahitimu 600,000 hadi 800,000 wanaoingia katika soko la ajira nchini.
Kwa kijana ambaye hana mahali pa kuishi, hajui atakula nini kesho, hana fedha za kununua nguo, kukata tamaa na kuamua kufanya lolote si kitu anachoweza kukifikiria mara mbili.
Kwa vijana wa kiume wapo wanaoamua kuwa wezi au matapeli huku wengine wakijikuta wakiwa walevi wa kutupwa au kuvuta unga kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na maisha magumu.
Utumiaji wa vilevi hivyo, umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza tatizo la afya ya akili kwa vijana wengine.

Kwa wasichana, ukosefu wa ajira, huwaingiza wengi katika wimbi la kutumia miili yao kujipatia kipato kutoka kwa wanaume. Wengine hujikuta wakiolewa mapema na hivyo kupoteza ndoto za kujiendeleza kielimu ili kujitegemea.
Mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini kwakuwa wasichana wadogo huzalishwa katika umri mdogo na wengine kukumbana na unyanyasaji wa nyumbani kutoka kwa waume zao.Katika maeneo ya vijijini ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo, ufugaji au uvuvi, baadhi ya wasichana waliolewa, hujikuta wakiachiwa familia zao kwa muda mrefu na waume zao wanaoenda kutafuta maisha. Baadhi ya wanaume hao huondoka kimoja na kuwaachia wake mzigo wa ulezi wa familia.
Hivyo, tatizo kubwa la ajira kwa vijana lipo kwa wale ambao hawana elimu ya kutosha kustahili kuajiriwa katika ajira rasmi. Kwa mujibu wa survey iliyofanywa na Restless Development, Tanzania ina takriban watu milioni 25 walio chini ya miaka 25 nchini. Hiyo ina maana kuwa karibu nusu ya watu wote nchini ni vijana.
Dunia nzima, vijana wamekuwa wakitambulika kwa kuwa na mchango mkubwa kuanzia katika upatikanaji wa uhuru enzi za ukoloni hadi katika kuvumbua teknolojia mpya na kugundua njia mpya za sanaa na muziki. Vijana ndio wanaolisukuma zaidi gurudumu la maendeleo kwa uchapakazi wao kutokana na miili na akili zao kuwa na uchangamfu zaidi.
Hata hivyo Tanzania ni nchi iliyo na matabaka yanayotokana na umri na jinsia huku vijana wakioneana kutopewa fursa katika mchakato wa maamuzi katika hatua za kijamii na hata katika serikali.
Ili kuwapa nafasi zaidi vijana katika nafasi za juu za maamuzi, vijana wanapaswa kutambua kuwa huu ndio wakati wao na sio kesho. Vijana wanatakiwa kwanza kujiamini wao wenyewe kuwa hakuna nafasi ya baadaye kwakuwa huu ndio wakati unaowaruhusu kuwa wabunifu zaidi kushawishi maendeleo.
Mawazo yao mapya na njia zao tofauti za kukabiliana na mambo, yataleta utofauti mkubwa wa sera, maamuzi na muelekeo wa serikali au taasisi mbalimbali.
“Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga Tanzania mpya, kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na vijana. Vijana wa Tanzania washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma. Tunaweza,” aliandika January Makamba kwenye mtandao wa Facebook.



VIJANA WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUSAKA MAISHA KUPITIA MFUMO WA TEKNOLOJIA AMBAYO INAWAWEZESHA KUWA WAJASILIAMALI, KATIKA NCHI HII YA TANZANIA, ZAIDI TUNAWEZA KUMUONA ANAVYOWEZA KUPAMBANA NA MAISHA. 

No comments: