Mfalme na Malkia wa Taarab, Mzee Yusuph na Khadija Kopa, ni miongoni
mwa wasanii wanaotarajiwa kupamba show ya Kili Music Tour inayodhaminiwa
na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager itakayofanyika leo katika Uwanja wa
Mkwakwani, jijini Tanga.
Malkia wa mipasho Khadija Kopa akihojiwa ndani ya Breeze FM Tanga
Wawili hao ni miongoni mwa wasanii wenye kupendwa hasa katika mikoa
ya ukanda wa Pwani na Tanga, huku wao wakiahidi kumwaga burudani ya
nguvu ikiwa ni ya mwisho kwa mikoani kabla ya kufungwa jijini Dar es
Salaam.
Joh Makini na G-Nako wa kundi la Weusi katika Interview
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema
jana kuwa, lengo la ziara hiyo yenye kauli mbiu ya ‘Kikwetu Kwetu’ ni
kukuza muziki wa ndani na pia kuwapa burudani wapenzi wa muziki mikoani.
“Ziara hii ina lengo la kuwapeleka wasanii kwa wananchi na pia ina
lengo la kukuza muziki wetu wa ndani ndio maana tulichagua kauli mbiu ya
kikwetu kwetu yaani tunajivunia kilicho chetu,” alisema Kavishe.
Rich Mavoko akiingia katika Tour Bus jijini Tanga
Show ya Tanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani, inatarajiwa kuanza
saa kumi jioni hadi usiku sana. Kavishe alisema kiingilio katika tamasha
hilo ni tsh 3,000 na kila anayeingia atapata bia moja ya Kilimanjaro
Premium Lager, lakini awe ametimiza au zaidi ya umri wa miaka 18.
Ben Pol akiwa Voice of Africa, Muheza Tanga akieleza namna alivyojiandaa
Mbali ya Mzee Yusuph na Khadija Kopa, wengine watakapamba shoo hiyo
ni Prof. J, Rich Mavoko, Ben Pol, Weusi na Ommy Dimpoz. Hii ni ziara
inayoratibiwa na makampuni ya East Africa TV na radio, Executive
Solutions, Aggrey and Clifford, Integrated Communications na Aim Group.
Ziara hiyo inatua Tanga ikitokea Mkoani Kigoma kabla ya hitimisho la aina yake litakalofanyika Septemba 6, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment