Je huu ni ukweli kwamba hakuna njia ya mkato kuelekea mafanikio?
Inawezekana unasema ‘Awali hujui mambo yanayoendelea na utabakia hivyo
hivyo’. Kuna kitu nimeendelea kujifunza kwa watu matajiri wanaochipukia
kwenye Forbes magazine na kwingineko.
Siku chache zilizopita katika Kongamano fulani ambako Mjasiriamali wa
Kenya Julian Kyula na Heshan De Silva waliongea kutokana na uzoefu na
historia ya Maisha yao. Kitu kimoja cha kufanana ni kutumia kile
ulichonacho na uweze kukiendeleza kufikia kule unakotaka.
Hakuna Njia ya Mkato kwenye Mafanikio; Kama kuna
kitu ambacho hatutaweza kuendelea ni
kupitia njia za mkato. Njia za
mkato haziwezi kujenga maendeleo yako wala hutoweza kuacha kitu
kiuchumi. Kwanini? Kuwa na fedha ambayo huna maelezo nayo au
haujaiwekeza kwenye njia sahihi ni kupoteza hiyo mali.
Mimi huangalia zaidi upande chanya zaidi kuliko upande hasi, kwa kila
mtu ambaye namtolea mfano naangalia upande chanya, kama una kitu hasi
juu ya yeyote huo sio upande wangu wa makala hii.
Kuna njia nyingi za utafutaji wa mafanikio “kama kupanda na kuvuna”
kitu ambacho watu wengi wanapenda, vilevile biashara za njia ya mitandao
ili upate kamisheni kwaajili ya watu wanaojiunga chini yako. Hizo
hazijawahi kuwa njia sahihi za kufanikiwa mara nyingi zinaishia
kutapeliwa.
Kufanya kazi kwa umakini na sio kwa nguvu. Umakini
unaozungumziwa hapa ni kuwa na watu sahihi au mtandao sahihi wa watu
kuhusu biashara au bidhaa unayoifanya. Umakini huo utakusaidia kufikia
malengo yako, haimaanishi kwamba hautakutana na vikwazo mbalimbali ila
je una umakini gani kupambana na vikwazo hivyo?
Inabidi Ukuze kitu ulichonacho. Watu wengi tunaogopa
kuchukua hatua ya kuamini kwamba kitu ulichonacho kinaweza kuwa kitu
kikubwa cha kuweza kukutengenezea ajira yako na watu wengine. Tunakuwa
na sababu nyingi na za kutosha kuonyesha kwamba haiwezekani. Ila ukweli
uko hivi kwako haiwezekani ila kuna mtu sehemu fulani usiyoijua wewe
kimewezekana. Hivyo inategemea mtazamo wako ukoje. Vitu vingi
tunavyovifanya sasa hivi wazee wetu hawajawahi kufikiri kwamba
vitawezekana lakini vinafanyika na wanaona vinawezekana, hivyo badilisha
unavyofikiri unaweza ukabadiisha matokeo ya vitu unavyofanya kila siku.
Nuia Kukua kimtizamo na kiutendaji.
Sisi sote ni matokeo ya maamuzi tunayofanya kila siku kuhusu maisha
yetu, hivyo mwenye maamuzi ni wewe mwenyewe kufanya kilicho sahihi au
kuamini na kufanya kulingana na habari za mtaani.
No comments:
Post a Comment