Kiba amesema mipango hiyo ilikuja kubadilika baada ya kugundua ngoma imekuwa kali bila Fally hivyo ikamlazimu kuiacha kama ilivyo na
kuandaa wimbo mwingine atakaomshirikisha star huyo.
“(Mwana) ilikuwa nifanye na Fally before, lakini sasa tulipoona nyimbo nimerekodi ikwa nzuri zaidi tukasema tusiiharibu anaweza akarekodi labda bahati mbaya ameharibu bahati mbaya amepatia kwahiyo nikamwandalia ngoma nyingine Fally,” amesema Alikiba kupitia XXL ya Clouds FM.
“kwahiyo ilikuwa imeandaliwa beat lakini sasa kwa utamu nilivyokuwa nimeuzidisha sana mle ndani mpaka tukaogopa kwamba Fally asije akapotea au akapoteza zaidi, lakini sikufikiria hilo, kitu cha muhimu ambacho nilifikiria kwamba ukiona nyimbo imekuwa nzuri zaidi sana, iache hivyo hivyo iende tutafute kingine.”
No comments:
Post a Comment