Baada ya uchumba wa Ciara na rapper Future kuvunjika, PAGE SIX imeripoti kuwa mwimbaji huyo wa R&B amemrudishia Future pete ya uchumba aliyomvisha.
Vyanzo vya karibu vimesema kuwa Ciara hana mpango wa kurudiana na Future, na hiyo ndio sababu ya
kuamua kumrudishia pete hiyo yenye thamani ya dola laki 5, ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 800.
“Friends of Ciara, who’s working on another album, tell us she’s “definitely not getting back together” with the rapper, and is focused on being a mom to their son, Future Jr.”
Future alimchumbia Ciara October 2013 na uchumba wao ulivunjika August 2014 ikiwa ni miezi mitatu toka wapate mtoto. Japo kuna ripoti zingine zilizotoka kabla ya hizi za sasa zilizodai kuwa, wawili hao wameamua kumaliza tofauti zao na kuanza kuishi pamoja tena ili kumpa malezi bora mtoto wao Future Zahir Wilburn.