Muigizaji wa filamu Blandina Chagula aka Johari amesema pamoja na kusikitishwa kutokana na bodi ya filamu nchini kuizua filamu ya ‘Sister Marry’ isitoke, amekula hasara kubwa.
“Unajua inauma sana, tumeshindwa kutetea filamu ya ‘Sister Marry’ kutokana na madai eti tumedhalilisha dini. Ina maana hawataki tuzungumzie maisha halisi kwenye filamu zetu? Mimi binafsi imeniumiza sana. Ile filamu imegharimu zaidi ya milioni 30, hebu angalia, Halafu inafungiwa ili isitoke kabisa! Kinachonisikitisha ni kwamba serikali yetu inashindwa kuangalia sisi tunavumbua baadhi ya maovu ya watu ambayo wanayafanya ili kuelimisha jamii. Kwahiyo imefungiwa na kukatazwa isitoke kabisa kwa sababu kuna mambo ya ukweli ambayo tumeyaonyesha. Tumefanya kila njia mpaka sasa hivi tumeshindwa, kwahiyo filamu ya Sister Marry haitatoka tena,” amesema Johari.