TAARIFA YA BODI YA WADHAMINI WA JOHA
TRUST KWA WAZAZI NA UMMA KUHUSU MCHANGO WA SHS BILIONI 1.617 KUTOKA KWA
BW. JAMES RUGEMALIRA WA TAREHE 12 FEBRUARI, 2014
1. Bodi ya Wadhamini ya Shirika la
Barbro Johansson Girls’ Education Trust (JOHA TRUST au BARBRO) inatoa
taarifa hii kutokana na utata
uliojitokeza kuhusu mchango wa Shs bilioni moja milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,0000/- ) tulioupokea kutoka kwa Bw James Rugemalira wa VIP Engineering and Marketing Limited.
uliojitokeza kuhusu mchango wa Shs bilioni moja milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,0000/- ) tulioupokea kutoka kwa Bw James Rugemalira wa VIP Engineering and Marketing Limited.
2. Mwanzilishi wa Shirika na Malengo
yake: Bodi ya Wadhamini BARBRO inachukua nafasi hii kufafanua kwamba
kiongozi wa Waanzilishi wa asasi yetu ni Mhe Profesa Anna Tibaijuka
ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Malengo na
madhumuni ya taasisi ya JOHA TRUST ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa
kike kwa kuwafadhili wasichana wenye vipaji lakini watokao katika
familia za kipato kidogo kusoma katika shule bora inazoziendesha.
3. Jina la taasisi ya JOHA TRUST
linatokana na uamuzi wa wanawake waanzilishi kumpa heshima Hayati Dr.
Mama Barbro Johansson (1912-1999) aliyewasili kutoka Sweden mwaka 1946
kama mmisionari na kuanzisha shule ya wasichana ya kati hapo Kashasha
Bukoba. Mwaka 1954 alijiunga na Mwalimu Nyerere kupigania uhuru na
baadaye kuwa raia wa Tanzania na Mbunge. Mwaka 1964 aliombwa na Mwalimu
Nyerere kujitolea kuwa Mwalimu Mkuu wa sekondari ya juu (High School)
pekee ya wasichana ya Tabora Girls iliyokuwa imekumbwa na utovu wa
nidhamu na kutaka kufungwa. Mama Barbro akafanikiwa sana kuigeuza shule
hiyo kiasi kwamba ilipata nishani ya UNESCO mwaka 1967. Mama Barbro
ndiye alianzisha elimu ya watu wazima nchini na pia ndiye alimuunganisha
Mwalimu Nyerere na wahisani kutoka nchi za Nordic ambazo zilianza
ufadhili wake katika Kituo cha Elimu Kibaha na Kituo cha Kilimo, Uyole,
Mbeya.
4. Shule za JOHA TRUST na Sura yake:
Shirika linamiliki na kuendesha Sekondari mbili nchini. Kwanza ni
Sekondari Bingwa ya Barbro iliyopo jijini Dar es Salaam. Ilianzishwa
mwaka 2000 ikiwa na wasichana 40 na hivi sasa wapo 632 wote wa bweni
katika kidato cha 1 hadi 6. Pili ni Kajumulo Girls’ High School iliyopo
Manispaa ya Bukoba. Ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wasichana 31 na hivi
sasa wapo 151 katika kidato cha 1, 5 na 6. Jumla shule hizi zina
wanafunzi 783 na waliomaliza ni 1,512. Wote isipokuwa 5 walifaulu
mitihani na kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbali mbali ndani
na nje ya nchi. Kwa kulingana na uwezo wa mfuko wa ufadhili, wasichana
453 sawa na asilimia 30% ya wanafunzi wamesaidiwa karo. Shule ya Barbro
imekuwa miongoni mwa shule kumi bora Tanzania (2010) na kwa wastani
inakuwa kati ya shule 50 bora katika mitihani ya taifa. Itambulike
kwamba mafanikio haya yanapatikana pamoja na shule kuwa na sera ya
kutowafukuza wanafunzi kwa misingi ya ufaulu wa mitihani ili mradi wawe
na nidhamu. Falsafa yetu ni kuwahimiza wanafunzi kuweka bidii kadri ya
uwezo wao, kujithamini na kujiamini katika maeneo wanayofanya vizuri.
Kipa umbele chetu ni maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja kwanza na sifa
kwa shule baadaye. Katika hali hii walimu hawana budi kufanya kazi ya
ziada.
5. Gharama za Uendeshaji na vyanzo
vyake: Tangu ianzishwe JOHA TRUST imetumia gharama ya Shs bilioni
thelathini na mbili (Shs 32,267,000,000/-) ambazo zimetokana na karo na
michango ya wazazi asilimia 37%; wafadhili wa nje asilimia 35%,
wafadhili wa ndani asilimia 7% na mikopo asilimia 21%. Kama taasisi
nyingi zinazotoa elimu, JOHA TRUST inakabiliwa na uhaba wa fedha na
ujenzi bado kukamilika. Shule inatoa huduma ya elimu bora na haifanyi
biashara kama wengi wasioelewa wanavyofikiri. Bila ruzuku na misaada
viwango vyake vya juu haviwezekani. Shirika la misaada la Sweden (SIDA )
ambalo limekuwa mfadhili mkubwa limekamilisha ahadi yake ya ufadhili wa
miaka 10 (2002-2012) lililopanga kwamba ingelitosha kusimika taasisi ya
JOHA TRUST na kuitaka ijitegemee. Hata hivyo SIDA imeacha utekelezaji
wa Master Plan ya BARBRO ya mwaka 2004 bado kukamilika. Jambo hili
limekuwa changamoto kubwa kwa Bodi kwa sababu katika Master Plan SIDA
ilipandisha viwango vya majengo kuwa juu kulingana na sifa na hadhi ya
Mama Barbro. Ikihitimisha ufadhili huo, SIDA ilihimiza Bodi kuhamasisha
michango ya ndani ili kujenga uendelevu na kukamilisha ujenzi wa Master
Plan hiyo.
6. Maombi ya Ufadhili: Kwa kuzingatia
ushauri huo wa SIDA, mwaka 2012 Bodi ilimtaka Mwanzilishi
(ProfesaTibaijuka) ambaye pia ni Mtafuta Fedha (Fund Raiser) wa JOHA
TRUST kuwaomba baadhi ya wafanyabiashara mashuhuri nchini kuunga mkono
shughuli za asasi yetu kwa michango. Bwana na Bibi James Rugemalira ni
miongoni mwa wafanyabiashara walioombwa mchango huo kwa barua ya tarehe 4
Aprili 2012 kupitia kampuni yao ya Mabibo Beer Wines and Spirits
Limited. Hatimaye mapema Februari 2014, bila kutaja ni kiasi gani, Bw.
Rugemalira alimjulisha Mwanzilishi kwamba yuko tayari kufanya mchango
ulioombwa na kumwagiza kwamba sharti ni yeye Mwanzilishi kufungua
account hapo Mkombozi Benki kuupokea mchango huo na kuchukua jukumu la
kuufikisha shuleni na kuhakikisha unatumika kama ilivyokusudiwa. Bw
Rugemalira alieleza hakutaka kuhangaika kuhamisha fedha kwenda benki
nyingine ambapo tayari kulikuwa na akaunti za shule.
7. Mchango wa VIP ulivyopokelewa: Kama
alivyotakiwa, Mwanzilishi alifungua account hiyo hapo Benki ya Mkombozi
tarehe 3 Februari, 2014 na kuupokea mchango huo wa jumla ya bilioni
moja, milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,000/=)
kwa niaba ya shule tarehe 12 Februari, 2014 kutoka kwa kampuni ya VIP
Engineering and Marketing.
8. Maamuzi ya Bodi: Bodi ya Wadhamini
BARBRO ilikaa katika kikao maalum tarehe 13 Februari, 2014 kupokea
taarifa ya mchango huo mkubwa kutoka kwa Bw. Rugemalira kupitia kampuni
yake ya VIP Engineering. Bodi iliukubali na kuamua mchango huo utumike
kulipa sehemu ya deni la shule hapo Bank M ambalo lilikuwa changamoto
kubwa. Kwa hiyo Mwanzilishi aliagizwa na Bodi kuhamisha fedha hizo
kutoka akaunti yake ya Mkombozi kwenda akaunti ya Bank M kulipia mkopo
huo. Hii inafafanua kwa nini fedha zilihama kwa haraka kutoka Benki ya
Mkombozi kwenda Bank M kwa wale wanaohoji suala hili.
9. Ulipaji wa Deni na Madai yaliyobakia:
Ili kutekeleza Master Plan, Julai 2011 JOHA TRUST ilikuwa imechukua
mkopo wa Shs bilioni mbili (Shs 2,000,000,000/-) hapo Bank M kwa ajili
ya ujenzi wa bweni kubwa lenye uwezo wa vitanda 163. Hadi kufikia tarehe
19/04/2014 mkopo huo ulipolipwa wote, deni hilo lilikuwa limezaa riba
na gharama nyingine na kuongezeka hadi kufikia takriban jumla ya Shs
bilioni mbili, milioni mia saba arobaini na moja, lhaki tatu sabini na
nne elfu, mia nne arobaini na nne (Shs 2,741,374,444/-). Kwa hiyo,
pamoja na ukubwa wa mchango wa Bw Rugemalira bado umelipia sehemu ya
deni hilo tu. Sehemu nyingine iliyobaki (Shs 1,124,274,444/-) imelipwa
kutoka vyanzo vingine vya mapato ikiwemo mkopo wa milioni mia mbili
tisini na moja, lhaki tatu sabini na nne, mia nne arobaini na nne (Shs
291,374,444/-) zilizotolewa na Mwanzilishi kulipa riba ya kila mwezi
wakati wa uhai wa mkopo huo. Ilikuwa maamuzi ya Bodi kupunguza madai
hayo ya Mwanzilishi kutoka takriban Shs milioni 291 na kubakia takriban
Shs milioni 174 . Kwa hiyo fedha zote alizozitoa Bw Rugemalira za Shs
1.617,100,000/- zilitumika kulipa mkopo na wala hazikutosha. Katika hali
hiyo, hisia na madai yanayotolewa kwamba Mwanzilishi alijinufaisha na
fedha hizo SI KWELI. Isingewezekana.
10. Ufadhili Endelevu wa Shule:
Itambulike kwamba hata kwa nafasi yake Mwanzilishi ni mfadhili na
mdhamini mkubwa wa JOHA TRUST kwa fedha zake binafsi. Bodi ilimwomba awe
analikopesha shirika letu na wafadhili wakipatikana tunamrejeshea fedha
zake polepole. Kwa mfano SIDA iliwahi kuridhia kwamba sehemu ya msaada
wake utumike kurejesha mkopo uliotolewa na Mwanzilishi wakati wa
kuanzisha shule kati ya mwaka 2000 hadi 2003.
11. Mchango wa VIP ulipokelewa kwa nia
Njema. Shirika halina utaratibu kuwahoji wafadhili wetu wa ndani au nje
kwanza kuthibitisha chanzo cha fedha zao wanazotuchangia. Misaada na
michango, iwe mikubwa au midogo, yote imekuwa ikipokelewa kwa nia njema
tukiamini pia inatolewa kwa nia njema. Tunaamini hivi pia ndivyo ilivyo
kwa asasi nyingine nchini na jamii kwa ujumla kwa mfano michango ya
maendeleo na hata harusi na shughuli nyingine kama hizo. Kwa kuwa
tulihakikishiwa na Benki ya Mkombozi kwamba fedha za Bw Rugemalira
zilikuwa zimelipiwa kodi, tulipokea mchango wake kwa furaha bila wasi
wasi wowote.
12. Michango ya kuendeleza shule siyo
zawadi binafsi kwa viongozi wake: Tunatambua kuwa sheria ya Maadili ya
viongozi huwataka kuwasilisha zawadi zote zinazozidi Shs elfu hamsini
(Shs50,000/-) kwa mwajiri wao. Kuna wanaodai Mwanzilishi amekiuka
maadili kwa kutouwasilisha mchango huo Serikalini. Pia kuna wanaohoji
kwa nini mchango mkubwa huo haukwenda kwenye jimbo lake la uchaguzi
(Muleba Kusini) ili kuendeleza shule za Kata. Wote wanakosea. Mchango
ulitolewa kwa shule ya JOHA TRUST na Mwanzilishi alipoufikisha kwetu
tuliupokea na kuutumia kama ilivyokusudiwa kwa shughuli za maendeleo ya
shule na kumwendeleza mtoto wa kike. Kufanya vinginevyo ndiko
kungelikuwa kukiuka maadili.
13. Umuhimu wa Uchunguzi: Kupitia
luninga tulifuatilia mjadala Bungeni Dodoma jioni ya Ijumaa tarehe 28,
Novemba, 2014 kabla ya kikao hicho kuvurugika. Tulishuhudia jinsi Bunge
zima lilivyoazimia kwamba vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake kuhusu
waliopata ͞mgao͟ ili kuondoa mashaka na taarifa kamili zipatikane ili
pale penye makosa hatua stahiki kuchukuliwa. Kwa hiyo, katika kikao cha
Bodi cha tarehe 2 Desemba, 2014, kilichoitishwa rasmi kujadili jambo
hili, kwa kauli moja tunatamka kwamba hatuamini kabisa na tunashindwa
kuelewa kwa nini Mwanzilishi wetu atakiwe kuwajibishwa nafasi yake
Serikalini kwa kuwa tu alipokea mchango wa shule kwa niaba yetu. Jambo
hili litatuchanganya na kutukatisha tama sisi wananchi wa kawaida
tunaojitolea kutekeleza shughuli mbali mbali za maendeleo hususan elimu.
Tunaamini hatua hiyo pia itafifisha juhudi za viongozi wengine wengi
wanaohangaika kuhamasisha michango ya shughuli mbali mbali za maendeleo
ikiwemo elimu, afya, maji, vijana, walemavu, watoto yatima, watoto
wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, wazee, wajane, n.k. katika taifa
letu changa. Tunaomba Mhe Rais alione jambo hili. Ikiwa michango ya
maendeleo inayopokelewa na viongozi kwa niaba ya wadau wao itatafsiriwa
kama zawadi zao binafsi kuna hatari kuzorotesha ͞harambee͟ za maendeleo.
Tunaamini ufafanuzi huu utatosha kuondoa utata katika suala hili ili
umma na viongozi wa ngazi za juu wapate ukweli juu ya jambo hili na
ushiriki wetu. Bodi yetu iko tayari kujibu maswali yoyote yanayoweza
kuulizwa ili kuondoa utata huu kabisa.
14. Shukrani kwa Wafadhili: Katika miaka
15 ya uwepo wa taasisi yetu (2000 -2014) , JOHA TRUST imepokea michango
jumla ya Shs bilioni 13.59 kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Wafadhili
wakubwa wa nje ni SIDA ambayo imetoa jumla ya Shs bilioni 8. 15 sawa na
asilimia 60% na JOHA TRUST Sweden Shs bilioni 1.79 sawa na asilimia
13.11%. Mwaka 2000 Serikali ya Tanzania chini ya Mhe Rais mstaafu
Benjamin Mkapa ilitoa ardhi ekari 50 kujenga shule ya Barbro jijini Dar
es Salaam. Mwaka 2005 kabla ya kuondoka madarakani Rais Mkapa alikuja
kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne kukagua maendeleo
yetu, akaridhika na kuchangia Shs milioni tano (Shs 5,000,000/-). Kwa
wahisani wa ndani ya nchi Dr. Reginald Mengi Mwenyekiti wa IPP
amechangia jumla ya Shs milioni 278 mwaka 2013 alipokuwa mgeni rasmi
kwenye mahafali ya kidato cha nne. Kwa hiyo alichofanya Bw James
Rugemalira ni sawa sawa na wahisani wengine waliotuunga mkono.
Tunawashukuru wafadhili wetu wote wa ndani na nje ya nchi kwa michango
yao na tunawaahidi kuongeza juhudi zetu za kumwelimisha mtoto wa kike na
kwa kufanya hivyo jamii nzima ya Watanzania.
15. Ujumbe kwa Wazazi: Kama
ilivyofafanuliwa tarehe 25 Septemba, 2014 katika mahafali ya kidato cha
nne, ni muhimu kwa wazazi na walezi kuyaelewa vizuri yaliyojiri katika
suala hili kuepuka upotoshwaji unaotokana na sababu za kisiasa dhidi ya
Mwanzilishi wetu. Pamoja na matatizo yaliyojitokeza hatujakata tamaa
katika juhudi zetu kumjengea uwezo mtoto wa kike. Tunawaahidi wazazi
ambao wamekuwa na wasiwasi kuhusu ufadhili wa watoto wao kwamba kazi
inaendelea kama kawaida. Hivi sasa wasichana 83 katika shule ya BARBRO
na wasichana 20 katika shule ya KAJUMULO wanasoma kwa ufadhili.
Tunawahakikishia wasichana wote hawa 103 ambao ni asilimia 13% ya
wanafunzi wote 783 tulionao wasiwe na wasiwasi bali kuendelea kusoma kwa
bidii. Hakuna binti mwenye ufadhili tayari atakayepoteza nafasi yake
katika shule zetu kwa sababu ya tukio hili. Tunachukua nafasi hii
kuhimiza michango kutoka kwa wafadhili wengine watakaoguswa na juhudi
zetu ili tuweze kuongeza uwezo wa kuwafadhili wahitaji wafikie asilimia
30% tuliyokusudia. Pamoja tuendelee kushirikiana katika kuendeleza elimu
na ulezi bora kwa mtoto wa kike. Kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere ͞Hasa wakati wa shida kukata tamaa ni dhambi
No comments:
Post a Comment