Tuko kwenye jamii ambayo tunaambiwa wewe ni mwanaume bila kujua
mwanaume ni nani na wajibu wake ni nini. Tumekua na kukuzwa huku tukiiga
na kujifunza kusiko rasmi kuwa mwanaume halisi.Kila mtu atakuja na
maana ya mwanamme halisi kulingana na tamaduni na alivyoambiwa na jamii
anayotoka. Je swali langu la msingi, Mwanaume halisi ni yupi?
Nilikaa sehemu na kujifunza kitu ambacho labda kinaweza kukusaidia
kama mwanaume mwenzangu. Kuna mambo matano ambayo yanafafanua mwanaume
halisi kama ifuatavyo;
Mwanaume halisi ni mtu anayechukua hatua
Hii inamaanisha unapokuwa mwanaume lazima
jjue kuwa
wewe uchukue hatua za msingi na madhubuti kwa ajili yako, kwa
jamii na familia. Usisubiri mtu mwingine achukue hatua fulani wakati
wewe upo, ni kitendo cha kujua maamuzi ya msingi na kuyafuata.
Mwanaume halisi huwajibika katika maisha yake
Tuko kipindi ambacho uwajibikaji umekuwa tatizo sana kwetu hivyo kuacha
mambo mengi yakiharibika. Jamii imewajibika katika vitu visivyo vya
msingi kwa familia zao na kushangaa mambo mbona hayaendi? Kuwajibika kwa
ajili ya amani, upendo na familia kwa ujumla. Mwanamme halisi hulisha
na kuitimizia familia yake mahitaji ya muhimu kama chakula , makazi,
elimu, msimamo wa kiimani na kufundisha maadili yaliyomema kwa familia
yake.Mwanamme halisi hutunza watoto aliowazaa na huonyesha upendo kwa
watoto hao, haachi watoto wake kila mtaa.
Mwanamme halisi huongoza kwa kujitoa kwa wale anaowaongoza.
Uongozi sio kutawala na kufanya kila mtu akuogope na afuate kila
unachokiamua, hapana mambo hayako hivyo. Ni uwezo wa kuwadaidia watu
wengine namna ambavyo wanatakiwa wawe au waende kwa staili gani kufika
kule kunakotakiwa. Kiongozi wa kweli lazima ajitoe kuhakikisha
anaowaongoza wanafika wanakohitajika kufika, kwa kutimiza haja zao,
kuwapenda na kutokua mbinafsi.
Mwanaume wa kweli anapenda uaminifu. Uaminifu ni
kitu ambacho wengi tumepigwa mchanga wa macho na hivyo kudhani ya kuwa
uaminfu hauhitajiki kwenye familia zetu au hata kwa wapenzi wetu kwa
wale ambao hatujaoa. Kuna mtu mmoja akasema unapokuwa mwaminifu unakuwa
na ujasiri wa kusema ninampenda mtu fulani ila usipokuwa mwaminifu hauna
ujasiri huo. Je kama wewe ni mwanamme halisi je ni mwaminifu? Najua
wengi tumekuwa na stori nyingi na kusema uaminifu hauwezekani ni ndoto
tu, lakini kitu kimoja unachotakiwa ujue kama wewe sio mwaminifu kwenye
mausiano yako au ndoa yako kuna watu ni waaminifu na ambao familia zao
zinaendelea kwa furaha na amani. Wewe ni kuchagua kusuka au kunyoa.
Mwanamme halisi anaacha kumbukumbu nzuri ya kizazi chake.
Unachotakiwa kujiuliza je wewe utaacha heshima gani kwa familia yako
siku ukiondoka? Au kitu gani kizuri ambacho baba yako alikiacha na
ambacho una ujasiri wa kukisema hadharani? Unaweka mpango gani wa kuacha
kumbukumbu nzuri juu ya familia yako na wewe mwenyewe?
Hivyo ni baadhi ya vitu nimejifunza sehemu fulani, je jamii zetu tnatambua mwanaume kama nani?