button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Tuesday, October 28, 2014

Vurugu zazuka Mkutano wa BAWACHA Muleba


Mkutano wa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee umeingia dosari baada ya
vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM kuingia na mabango yao katika mkutano uliokuwa ukifanyika kijiji cha Kyamiorwa kata Kashalunga wilayani Muleba na kusababisha vurugu.
  
Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema Halima Mdee alipokelewa jana katika kijiji cha Kyamiyorwa na kufanya mkutano na wananchi katika kijiji hicho ambapo vijana wanne wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM waliingia katika mkutano huo huku wakiwa wameshikilia mabango yao na kusababisha vurugu katika mkutano huo, vurugu hiyo zimetulizwa na jeshi la Polisi na mpaka sasa jeshi la Polisi lina mshikilia kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Mansud Amri ambaye ametajwa kuhusika katika kufanya vurugu hizo.
  
Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee amewataka vijana kutotumiwa na wanasiasa wanao lenga kuvuruga amani ya nchi na badala yake watulie ili kujenga taifa lenye amani na utulivu.
  
Nao baadhi ya wafuasi wa chama hicho akiwemo mbunge wa viti maalumu Conchester Rwamlaza wamewataka wananchi kutoiunga mkono Katiba Mpya na akaongeza kuwa wananchi wanatakiwa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuhakikisha wana chagua viongozi bora ambao wataliongoza taifa hili kwa umakini.

No comments: