Rapper Shetta amedai kuwa anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Shikolobo’ aliomshirikisha msanii wa Nigeria.
Akizungumza na Global TV, Shetta amesema wimbo huo upo tayari na anachokisubiria ni maandalizi ya mwisho pamoja na uingizaji wa sauti kwa msanii wa Nigeria.
“Nizungumze kwamba kuna project mpya inakuja nilitakiwa niende Nigeria ila bahati mbaya mambo ya Ebola Ebola haya, serikali nahisi imepiga stop kidogo kwenye safari za kutoka lakini project ipo na kuna collaboration kubwa nitaifanya na Mnigeria mmoja surprise sasa hivi siwezi kumtaja. Afrika soko lipo lipo kule hata rotation ya muziki tunaiona. So ni vizuri penye nafasi tukaitumia. Ngoma nishafanya tayari kuna vitu vinarekebishwa inatumwa na jamaa aingize aje hapa,” alisema Shetta
Pia Shetta alizunguzia connection ya kufanya ngoma na msanii huyo pamoja na jinsi alivyomlipa.
“Ina depend the way ukaribu wenu the way unawasiliana vipi? Mimi hapa ameniconnect Diamond kwasababu sasa hivi Diamond when you talk about about Africa, East africa inamzungumzia Diamond kwahiyo ana connection nyingi. Nisivunge, Diamond amenisaidia hilo. Kwahiyo ngoma ipo tayari inaitwa Shikolobo, ikiwa tayari itazungumziwa.”