Mrembo kutoka Temeke, Sitti Mtemvu ametwaa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014, katika shindano lililofanyika Jumamosi, usiku wa (11 October) katika ukumbi wa Mimani City jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu (katikati) akiwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima pamoja na watatu Jihan Dimachk
Kutokana na ushindi huo Sitti amejishindia zawadi ya shillingi milioni 18 na pia kupata fursa ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye shindano la Miss World 2015.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Lilian Kamazima na Jihan Dimachk akiambulia nafasi ya tatu.
Nafasi ya nne ilienda kwa Dorice Mollel na Nasreen Abdul akishika nafasi ya tano. Tazama picha za matukio mbalimbali pamoja na show ya Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee.
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa akiwa amekalia kiti chake kabla ya kumkabidhi miss mpya