Mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba, Jack Ma amekuwa mtu tajiri zaidi nchini China. Jack ana utajiri wa dola bilioni 25.
Jack Ma
Ma, aliyeanzisha kampuni ya biashara ya mtandaoni ya China kutoka kwenye nyumba ndogo aliyokuwa akiishi, amekamata nafasi hiyo kwa mujibu wa Hurun Report. Amemzidi mwenyekiti wa Wanda Group Wang Jianlin, mwenye utajiri wa dola bilioni 24.2 na mmilikiwa wa kampuni ya nishati ya Hanergy, Li Jejun mwenye utajiri wa dola bilioni 20.8.