Ana miaka miwili tu, lakini North West ameanza kuhudhuria fashion show za kimataifa tena katika mstari wa mbele. Weekend iliyoisha, mtoto huyo wa Kanye West na Kim Kardashian ameshuhudia cat walks za warembo mbalimbali akiwemo mama yake mdogo, Kendall Jenner kwenye Paris Fashion Week na pia kwenye show ya Givenchy jijini Paris, Ufaransa.
Hata hivyo katika picha nyingi, North alionekana kutofurahishwa na huenda alikuwa anataka kwenda kulala kama watoto wengine wa umri wake? Ni sawa kwa Kanye na Kim kumpeleka mtoto wao kwenye show za aina hiyo tena usiku kwa umri wake? Tazama picha hizi.