Kutofanyika kwa show ya kimataifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na
mashabiki wengi wa Diamond jijini Stuttgurt, Ujerumani na kusababisha
uharibifu mkubwa, kulichukuliwa na watu wengi kama ajali kazini.
Sababu za Diamond kuchelewa kupanda stejini kulikotokana na kudai
alipwe fedha yake iliyokuwa imesalia kwa
promota, ilikuwa ya msingi kabisa. Na pia kampuni yenyewe iliyoandaa show hiyo ilieleza kwa urefu kilichosababisha na pia kuahidi show ya bure kwa mashabiki wa Diamond.
promota, ilikuwa ya msingi kabisa. Na pia kampuni yenyewe iliyoandaa show hiyo ilieleza kwa urefu kilichosababisha na pia kuahidi show ya bure kwa mashabiki wa Diamond.
Hilo lilipita na kila upande ukaganga yajayo. Ijumaa hii Diamond
alikuwa afanye show nyingine jijini London, Uingereza. Bahati mbaya show
hiyo ambayo yeye mwenyewe kama kawaida yake aliipigia promo sana,
haikufanyika. Kama ilivyokuwa ya Ujerumani, mashabiki walimsubiri staa
huyo kwa masaa kibao wasimuone akitokea. Baada ya kuonekana kunakucha
bila dalili ya Diamond kupanda jukwaani, wengi walianza kudai
warudishiwe fedha zao. Na kwa mujibu wa mtu aliyekuwepo kwenye show
hiyo, polisi walisaidia kurejesha amani katika ukumbi huo, lasivyo
yangetokea kama ya Ujerumani.
Pia anadai kuwa promota wa show hiyo alikamatwa.
“I was there brov it was maad trust me, even police got involved
with that shit, they had to calm people down until seven in the morning,
people wanted their money back he I’ll pay the price cause he got
arrested,” ameandika.
Diamond amemtupia lawama promota huyo ambaye si mara ya kwanza kufanya naye kazi na kumuita tapeli.
“Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!….kuweni makini sana na promoter
huyu (Victor – Dj rule) mnaposikia kaandaa show, party au Hafla
yoyote…ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwasababu ni tapeli….
si unajua aisifiae mvua imemnyeshea… basi mie nimeloa kabisa.”
Pamoja na kwamba Diamond hana makosa katika hili, hawezi kukweka
lawama kutoka kwa mashabiki wake walio na kinyongo naye. Shabiki
hatotaka kujua makubaliano kati ya msanii na promota. Anachojua yeye ni
kuwa show ilitangazwa kuwa itafanyika na yeye akanunua tiketi kuja
kushuhudia.
Si kazi yake kutaka kujua kama msanii amelipwa fedha yake ama lah!
Kama Diamond alikuwa anamfahamu vyema DJ Rule kuwa si mwaminifu, kwanini
alikubali kufanya naye show? Sijui makubaliano yao yalikuwa vipi,
lakini kwanini alikubali kulipwa fedha nusu kabla ya kutumbuiza?
Ni yaleyale kama ya Ujerumani.
Ni yaleyale kama ya Ujerumani.
Wengi tunamchukulia Diamond kama mfano wa msanii wa Tanzania
aliyefanikiwa na tunategemea kuwa makubaliano yake yanapaswa kuwa kwamba
promota anatakiwa kumlipa ama fedha nusu, robo tatu au fedha yake yote
(kama anamuamini) na kusaini mkataba unaowafunga wote. Mara nyingi
mikataba husema fedha iliyosalia inatakiwa imfikie msanii wiki moja ama
siku chache kabla ya show. Wengine hukubaliana fedha hiyo alipwe msanii
pindi anapowasili katika mji huo ama anapofika hoteli.
Ninafamu kuwa Diamond na timu yake wako smart mara nyingi lakini
nashindwa kupata jibu la kwanini makosa kama haya yanaendelea kutokea
tena katika show za kimataifa. Kuna uwezekano mkubwa kama hajapoteza
mashabiki wengi, basi heshima waliyokuwa nayo kwake imepungua.
Yeye na timu yake wanapaswa kuwa smart na kusaini mikataba ya show
isiyokuwa na ahadi za kupeana fedha iliyobaki siku ya show. Promota
wanapaswa kujipanga na wanapotafutwa na promota wenye longolongo wasiwe
na aibu kuwakatalia moja kwa moja kutunza heshima yao.
Matukio kama haya yanaweza kuwa mabaya kwa biashara pia kwakuwa
baadhi ya promota wa kimataifa hawapendi kufanya kazi na wasanii wenye
CV mbaya katika show zao zilizopita.
Haya ni baadhi ya maoni ya watu mbalimbali yanayofanana kiasi na ya kwangu.
kiswigogodfrey
Play back concert 2 times inabuma hiyo ni kukosa management imara yenye kusimamia mikataba yako. Umetoka bongo hadi UK bila kujua mikataba yako. Hilo fans wako haliwahusu wao ni burudani ndio haki yao hayo mengine utajijua na promota wako. Na kama jamaa amekupiga kama ulivyo post ni vzr ukafuata taratibu za kisheria ndio zitoe hukumu na ukishinda ndio umwanike kwenye social network.Kama hujafanya hivyo tegemea kesi ya madai kutoka kwa mshikaji ingawa umeshapata hasara kwa kukosa umakini na management yako, it’s over.
Play back concert 2 times inabuma hiyo ni kukosa management imara yenye kusimamia mikataba yako. Umetoka bongo hadi UK bila kujua mikataba yako. Hilo fans wako haliwahusu wao ni burudani ndio haki yao hayo mengine utajijua na promota wako. Na kama jamaa amekupiga kama ulivyo post ni vzr ukafuata taratibu za kisheria ndio zitoe hukumu na ukishinda ndio umwanike kwenye social network.Kama hujafanya hivyo tegemea kesi ya madai kutoka kwa mshikaji ingawa umeshapata hasara kwa kukosa umakini na management yako, it’s over.
jamal_huwel
Men mara ya pili hii hebu badilisha system ya mikataba yako. Pokea
angalau 60% of the cash kabla ya shoo. Watakuharibia mtaalamu wetu
tutakosa talent yako tena
Allykikasha
PLZ PLZ PLZ READ THIS….DIAMOND wewe ushakuwa msaani wa kimataifa na
watu nao wanakufahamu,, jaribu kutafuta timu ya uhakika mtu anayejua
ishu ya marketing professionally,, uwe na mwanasheri hata yule wa
kumlipa tu pale unapoingia mkataba,, achana na waki BABU TALE wao
umeneja wao ni wa show za mikoani tuu,, then hana creativity yoyote
zaidi ya kuwanufaisha,, jaribu now to change,, uwe na watu wenye uwelewa
na kitu unachokifanya,, Germany imetokea ,, then BAB TALE anasema eti
imesaidia kukutangaza,, very stupid comment then ISSUE SIO PROMOTERS
ITAFIKIA SIKU FANS NOW WATAONA KILA SHOWS ZAKO NI ZA KITAPELI ,, PEOPLE
THEY CHANGE.
carryandy
Acha kuwatangazia mashabiki wako show kabla hujalipwa hela kamili,
vinginevyo unajiharibia biashara 2nd time hii, hujajifunza tuu? Na sijui
kama unakuwa na makubaliano ya maandishi kabla hujajiingiza kuwambia
fans wako utkuwa somewhere. , jipange utaja pata matatizo makubwa nchi
za watu hizo oh!
rayna_rayna_
Mmmhh um not sure kama anaweza kukufanyia ivyo maybe umeenda bila
contract ndo mana imetkea yote..next tym jipange na team yko najua jamaa
ni mtu mkubwa and also unaweza kwenda mshitaki ubalozini kwa
kukupotezea mda na kukupotezea issue maybe it will help
callyrissanen
Pia kuwa makini chibu. Hao police wa nchi za wenzetu wakifanya
mawasiliano unaweza hata huko germany ushindwe kufanya show. Tafuta
mwanasheria wa hiyo mikataba yako. Na uwe unamaliziwa kulipwa pesa za
show unapofika tuu kwenye nchi husika, msisubiri hadi muda wa onyesho
ndio muanze kudaiana. Inakuwa rahisi kutoa tamko kwa mashabiki mapema
kama hutohudhuria mapema iwezekanavyo ili wasisumbuke
irymamur_de_star
Inaonekana management yako haipo makini kabisa kwan inatokea nn??
hadi mtu anakutapeli cc mashabiki zako tunaumia xana kuckia ivyo na
maswal mengi juu ya hilo kwan thamani yako ya show za nje inapungua xaxa
kuwa makini na hao bakoharam sio watu wazuri kwako na huyu jamaa xaxa
mi sioni kazi yake @babutale mi nakupa pole xana kwailo!!!! ila
hujafafanua vzur juu ya hilo tujue ilikuaje yani tujue mwanzo mwisho kwa
maelezo kwan tunahaki kama mashabiki zako pendwa!!!!
No comments:
Post a Comment