Friday, January 9, 2015
Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika Yanyakuliwa na Yaya Toule, ambapo ni mala yake ya nne kukanyakua tuzo hiyo!
Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kutajwa na shirikisho la soka barani Afrika kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa mwaka wa nne mfululizo.Toure mwenye umri wa miaka 31,aliteuliwa baada ya kucheza kwa kujitoa na kuleta ushindi katika Premier League na League Cup, na pia alijitoa kuisaidia Ivory Coast kuingia katika kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika baadaye mwaka huu.
Toure amewapiku mshambuliaji kutoka Gabon, Pierre Emerick Aubameyang na golikipa mnigeria Vicent Enyeama. Mwaka jana Toure alikuwa mwaafrika pekee kati ya wachezaji 23 duniani waliotajwa kuwania tuzo ya FIFA ya Ballon D’Or.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment