Rappers wa kundi la Mapacha, wamesema kwa sasa wameamua kufanya kazi
na wana amani moyoni baada ya kusuluhisha ugomvi wao na Clouds FM na
kutoa ngoma zao mbili.
Mapacha
Akiongea na Bongo5 member wa kundi hilo, Dotto aka D wa Maunjanja Saplayaz, alisema wao na Vinega bado wana uhusiano mzuri.
“Unajua kuna wengine ni ndugu pale unajua hizi na itikadi tu
zimebadilika lakini tunasalimiana kama kawaida. Unajua tunafanya mambo
kwa manufaa ya maisha yetu. Tokea tumemaliza tofauti zetu na uongozi wa
Clouds Media Group tumepata changamoto hasa kwa wale mashabiki wachache
wasiopenda maendeleo na wasioelewa. Unajua kuna watu wengine wanapenda
kuona nyie mpo kwenye matatizo kila siku inapotokea mmepata afadhali
unakuta hapendi anataka kuona mnataabika tu kila siku. Sasa hivi
tunafurahi kwakweli maana tunapa show kama hii ya Fiesta. Unajua unapo
kuwa msanii show ni muhimu sana na unapopata show ndo mambo mengine
yanaenda.”
Kwa upande mwingine Mapacha wamesema hiphop bado ni muziki unaopendwa zaidi.
“Unajua hiphop ndo muziki ambao umekuwa ukifanya vizuri siku zote
hata kwenye show ndo muziki ambao umekuwa una amsha amsha. Hii miziki
mingine inakuja na kuondoka lakini hiphop yenyewe ipo palepale. Angalia
hata wasanii wengi wanaokuja bongo kwenye show ni wa hiphop. Kwaihyo
inaonyesha kabisa hiphop ndo muziki unaofanya vizuri. Na sasa tuna
mpango wa kufanya video ngoma zetu hizi mbili maana tunajua tuna deni
kwa mashabiki wetu. Kwahiyo wasijali video zinakuja muda si mrefu.”
No comments:
Post a Comment