Msanii wa longtime kwenye familia ya Bongo Flava ambaye hujiita
muasisi wa muziki huo, Dully Sykes amewataka Diamond na Alikiba kuweka
tofauti zao na kufanya kazi pamoja.
Dully amedai kuwa Alikiba na Diamond wanatakiwa wafanye kazi waweke
tofauti zao pembeni na waingize hela. “Hivi we unadhani itoke nyimbo ya
Alikiba na Diamond si itakuwa hatari sana! Maana hiyo ngoma itakuwa
gumzo na pia wata watawafurahisha mashabiki wao. Huo ndo ushauri kwa
wadogo zangu,” amesema Dully.
Katika hatua nyingine Dully ameiambia Bongo5 sababu za kutofanya
vizuri kwa nyimbo zake za sasa. “Unajua nyimbo yangu kama ile ya “Joka”
haikufanya vizuri kwakuwa watu walihisi kama nimemdiss mtu ndo maana
haikufanya vizuri. Kwa wimbo wa “Binti Spesho” nao ulishindwa kufanya
vizuri hasa ilivyofungiwa video yake lakini sasa wimbo wa ,’Togola’
unafanya vizuri nadhani pia umetoka kipindi kizuri na pia video yake ipo
tayari inatoka muda wowote kuanzia sasa.
Kuhusu kazi yake kama mtayarishaji wa muziki, Dully amedai kuwa anazidi kuifurahia.
“Tokea nimekuwa producer naenjoy sana maana napenda sana kazi ya kuwa
producer sasa hivi kuliko hata kuimba. Na pia sasa nimeshafanya kazi
kadhaa za wasanii wakubwa zinakuja kama ya Chidi Benz vile imeshatoka na
kuna zingine zinakuja. Unajua sasa hivi studio yangu ina vyombo vipya
vya kisasa na pia ntakuwa narekodi live yaani napiga vyombo vyote.”
No comments:
Post a Comment