Msanii mkongwe wa filamu nchini Emmanuel Myamba, amezungumzia bajeti
ya harusi yake iliyodaiwa ilikuwa ya kifahari pamoja na maisha yake
mapya baada ya kufunga ndoa.
Pastor Myamba akiwa na mke wake Praxceda
Myamba ambae amefunga ndoa na mwanadada Praxceda huko visiwani
Zanzibar mwanzoni mwa mwezi August, ameiambia Bongo5 kuwa hakutegemea
kama ndoa itakuwa kubwa kama ilivyokuwa.
“Namshuru mungu ndoa ilipita salama kama ulivyosikia, unajua budget
ya ndoa sikufufichi ilikuwa kubwa ila kusema kwamba ni shilling fulani
nitakudanganya, kamati ndo ilikuwa inajua kila kitu ila ndoa ilikuwa
kubwa sana, dah kusema kwamba ndoa ilikuwa ya milioni 100 au pungufu
nitakuwa sikutendei haki kwa sababu budget sijui ilikuwa kubwa kiasi
gani, nawashukuru sana wasanii wengangu ,ndugu, jamaa na marafiki
waliyowezesha harusi ikawa kubwa, pia kuna dada yangu ambaye
alinizawadia gari na vitu vingine” Alisema Myamba.
Pia Myamba amesema baada ya kuachana na ukapela kuna mambo mengi yamebadilika katika maisha yake.
“Baada ya kuoa najiona mwepesi, unajua maisha ya ubachela yana tabu
zake ila sasa hivi nipo safi maisha naona mazuri, kazi zinaenda vizuri,
sijawai kuwa na mtoto nazani sasa hivi ndiyo muda muafaka mungu
akipenda” Alimalizia Myamba.
Zawadi kutoka kamati ya maandalizi
Emmanuel Myamba akiwa na mke wake wakati wa kufunga ndoa huko visiwani Zanzibar
No comments:
Post a Comment