Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Apple Tim Cook ametangaza kuwa ni shoga na kwamba anajivunia kuwa hivyo.
Cook alitoa tamko hilo ili kujaribu kuwasaidia watu wanaong’ang’ana
kutangaza jinsia zao katika ripoti iliochapishwa katika gazeti la
biashara la kila wiki la Bloomberg. Wiki hii Cook alitoa changamoto kwa
jimbo lake la Alabama kuhakikisha kuwa haki za mashoga na wale
wanaobadili jinsia zinaheshimiwa.
“Mimi sijitambui kama mwanaharakati,lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine”,alisema Cook.
“Kwa hivyo iwapo watu wakisikia kwamba mimi ni shoga kutawasaidia
baadhi yao ,ama kumpa faraja yule anayejisikia mpweke ama kuwashinikiza
wengine kupigania haki zao,basi afadhali kutangaza maisha yangu ya
faragha,”aliongezea.
Cook amesema amekuwa wazi kuhusu hali yake na watu wengi wakiwemo
wafanyakazi wenzake katika kampuni ya Apple,lakini hilo halikuwa chaguo
rahisi kutangaza hadharani kuhusu hilo.
No comments:
Post a Comment