Kuwa mjinga katika ufanyaji wako wa mambo Wewe kama ni msanii umekuwa ukifikiri watu wanapenda kuchelewa kwako kufika kwenye show ambayo umealikwa, unapoteza thamani ya kazi yako.Kitu unachotakiwa kujua ni kwamba watu wanataka kukuona kwa wakati uliotajwa, na wanategemea uimbe kwa kiwango cha juu bila kuwafanyia ujinga au kuimba na kufanya show chini ya viwango.
Kushindwa kuweka muziki au sanaa yako kitaaluma zaidi. Waimbaji wengi au wasanii wengi wanashindwa kuzingatia sanaa yao kuwa taaluma yao. Unatakiwa kujua wewe kama msanii unatakiwa kufanya nini kila siku kuboresha sanaa yako kitaaluma. Inamaanisha unagusa hisia gani kwa wateja wako? Kushindwa kupangilia maisha yako ya muziki ni kupanga kushiwa kwenye muziki.
Kulewa sifa, matumizi ya pombe kupindukia pamoja na madawa ya kulevya Tuko kwenye jamii ambayo hakuna mtu anayeweza kukwambia ukweli kwa sababu wanaogopa kukufuatilia maisha yako binafsi. Ni kweli ni maisha yako binafsi lakini unachotakiwa kujua kuhusu maisha yako binafsi ni kwamba taaluma yako ya muziki unataka ifike wapi? Hata kama una muziki mzuri kiasi gani, pombe na madawa ya kulevya yanaua huo muziki bila ya wewe kujua na mwisho wa siku inabaki historia ya jina lako.
Unapokuwa mlevi na mtumiaji wa madawa ya kulevya, utashindwa kuimba jukwaani kwa kiwango kinachihitajika, utashindwa kutokea kwenye mahojiano kwa wakati na kibaya zaidi mwili wako na sura yako inaonekana kama kinyago. Unakuwa huna thamani tena ya utu wako mbele ya jamii.
Kutengemea sana mameneja uchwara badala ya kujenga taaluma yako ya sanaa na muziki. Unapotegemea watu wengine unaweza kusahau jukumu lako la kuimarisha muziki wako. Unahitaji kuwa makini na watu unaofanya nao kazi na wanakusaidia kufanya nini? Je wanajenga taaluma yako ya muziki au wanakutumia?
Kuanza kwa hela zaidi bila kuonyesha ubora wa kazi yako Hii haimanishi ufanye show bure au inamaanisha kulipwa kulingana na ubora wako. Na unahitaji kufahamu wapenzi wa muziki wako wanakuonaje? Je wako tayari kulipa shilingi ngapi kwa kazi zako? Na hutakiwi kutoa nyimbo nyingi za bure, unakuwa unajishushia hadhi.
Kuwa na mashabiki wenye fujo mashabiki wenye fujo wanakuponza wewe na taaluma yako. Hawa watu wanaweza kukusababishia hasara hasa kwa vitu na mali za watu kwenye show zako. Unahitaji kuwasoma mashabiki zako na kujua ni wa aina gani na kwanini wanafanya wanachokifanya kama kina madhaRa kwenye taaluma yako angalia namna ya kurekebisha.
Kuhonga ili ukafanye show Kumbuka watu wanaotambua muziki wako ni wasikilizaji , hivyo kama kazi yako ni nzuri watu watakufuata na kufanya kazi na wewe kama una muziki mbovu unapoteza muda na lazima mziki wako utakufa.
Kufanya rekodi wakati umelewa au kutumia madawa Kumbuka muziki unaofanya utaathiri vizazi vingi baadaye hivyo kama haukuwa halisi unatangeneza feki nyingi kama za wewe uliyonayo.