Jumamosi iliyopita, Oktoba 25, 2014
ilikuwa ni Siku ya Msanii Duniani ambayo kwa mara ya kwanza, Tanzania
iliiadhimisha siku hiyo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Gharib Bilal.
Siku hiyo ilipambwa na matukio kibao nyuma na mbele ya pazia, ambapo kubwa lilikuwa ni la Jokate Mwegelo ambaye alikuwa miongoni mwa ma-mc wa shughuli hiyo ya kitaifa, kumfagilia waziwazi msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwamba hakuna kama yeye, Ijumaa Wikienda lilikuwa ndani ya nyumba na kunasa matukio lukuki yaliyojiri.
JOKATE: HAKUNA KAMA DIAMOND
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, Jokate alimfagilia waziwazi Diamond na kusema hakuna msanii anayeweza kumiliki jukwaa kama yeye.Sifa hizo alizozitoa Jokate kwa Diamond, zilisababisha ukumbi mzima ulipuke kwa kelele hasa ukizingatia kuwa wawili hao walishawahi kuwa wapenzi ila wakatengana na kile kinachodaiwa kuwa ni maneno ya watu.
Ukichanganya na kilichotokea kwenye Serengeti Fiesta 2014 ambapo Diamond ‘alikula za uso’ ukilinganisha na mpinzani wake, Ali Kiba ambaye alishangiliwa kwa nguvu, kitendo cha Jokate kumnadi Diamond jukwaani kilizidi kutengeneza vichwa vya habari.
DIAMOND ASAFISHA NYOTA
Baadaye Diamond aliangusha Number One na Mdogomdogo ambazo ziliwafanya watu wachizike hivyo kudaiwa kusafisha nyota yake iliyochafuka hivi karibuni kwenye Tamasha la Fiesta katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar alipozomewa.

No comments:
Post a Comment