Waandaji Miss Tanzania, Lino International wanakutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuzungumzia skendo ya umri wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu. Swali ni Je! Atavuliwa taji hilo?
Wengi wanahoji umri halisi wa Bi Sitti Mtemvu wakisema
alidanganya. Lillian Kamazima alikuwa mshindi wa pili, ambapo Jihhan Dimachk alishika nafasi ya tatu.
Mara baada ya kutwaa taji hilo kumeibuka utata juu ya umri wa Miss Tanzania 2014.
Habari zimezagaa katika mitandao ya kijamii, ambapo anatuhumiwa kudanganya umri wake. Kuna taarifa zinasema Bi Sitti alitaja kuwa ana umri wa miaka 18 huku vitambulisho vyake vinaonesha kuwa ana miaka 26.
No comments:
Post a Comment