Mshindi wa Serengeti Super Nyota 2012 kutoka mkoani Mbeya, Neylee amesema wimbo wake mpya ujao ‘Hasara Roho’ unaelezea changamoto mbalimbali za maisha ya binadamu na jinsi ya kuachana nazo.
Muimbaji huyo ameiambia leokwetu kuwa
katika maisha ya binadamu kuna vitu unaweza kukutana navyo na vikakuvunja moyo.
“Hasara Roho ni wimbo ambao kwanza unajieleza katika hali ya kawaida,” amesema. “Hasara Roho ni kama kulipotezea jambo ambalo lilikukwaza, sasa unaamua kuachana nalo kabisa. Sio mimi tu kila binadamu anapitia changamoto, sema tunapambana nazo na kuacha maisha yaende mbele,kwahiyo wimbo utatoka hivi karibuni.”