Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere amejiuzulu wadhifa huo. Steve ametangaza uamuzi huo kupitia Instagram na pia kuithibitishia Bongo5.
“Unajua nimeona bora nijiuzulu ili tusije kuvunjiana heshima hayo ndo maamuzi niliyoamua nitabaki kuwa mwanachama wa kawiada tu kama wengine,” Steve ameiambia Bongo5.
Awali kupitia Instagram aliandika:
Napenda kuwashkuru ndugu zangu wote wasaniii wenzangu kaka zangu mama zangu rafiki zangu mimi pamoja na family yangu nimeamua kujiuzuru uongozi wa bongo move nabaki kuwa mwanachama wa kawaida naimani tulifurahi pamoja tukauzunika pamoja na daima tutakuwa pamoja
Uamuzi wa Steve Nyerere umepokelewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa filamu nchini na wengi wamemtaka kutofanya hivyo huku wakitaja‘majungu’ na kusemwa kama chanzo cha yote
No comments:
Post a Comment