Tanzania inashutumiwa kurejesha mpango wa kuwahamisha wamasai 40,000
katika eneo waliloishi kwa miaka na miaka, ili kuipa eneo hilo familia
ya kifalme ya Dubai kwaajili ya kuwinda wanyama.
Mwaka jana serikali ilidai kuahirisha mpango wa kutenga eneo la
kilomita ya mraba 1,500 zinazotengenisha mbuga ya wanyama ya Serengeti
kwa matumizi ya uwindaji wa biashara utakaofanywa na kampuni yenye makazi
yake kwenye falme za kiarabu, Ortelo Business Corporation (OBC).
Na sasa gazeti la The Guardian la Uingereza na mengine, yameandika kuwa mpango huo umerejea na wamasai
hao wameamrishwa kulihama eneo hilo kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Wawakilishi wa wananchi hao wanakutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
bungeni Dodoma kuelezea hasira yao.
Wanadai kuwa kuondolewa kwenye ardhi hiyo ni kunyang’anywa kwa urithi wao na maisha ya watu 80,000 yataathirika. Eneo hilo ni muhimu kwa malisho ya mifugo ya wananchi hao wanaoishi kwa kutegemea ufugaji.
Wanadai kuwa kuondolewa kwenye ardhi hiyo ni kunyang’anywa kwa urithi wao na maisha ya watu 80,000 yataathirika. Eneo hilo ni muhimu kwa malisho ya mifugo ya wananchi hao wanaoishi kwa kutegemea ufugaji.
Serikali itawalipa shilingi bilioni moja kama fidia ambazo wamasai wamezikataa.
“Nahisi kusalitiwa,” mratibu wa kikundi cha Ngonett Samwel Nangiria ameliambia The Guardian.
“Bilioni moja ni ndogo sana huwezi kulinganisha na ardhi. Imerithiwa.
Mama na bibi zao wamezikwa kwenye ardhi ile. Hakuna cha kulinganisha
nayo.”
Msemaji wa wizara ya Maliasili na Utalii, ameliambia gazeti hilo kuwa
hana taarifa kuhusiana na mpango huo.
No comments:
Post a Comment