Msanii mkongwe wa filamu nchini, Jacob Stephan aka JB amewataka wasanii wa filamu kuacha mara moja kuwasema vibaya viongozi wao.
Akizungumza na Bongo5 leo, JB ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa Bongo
Movie Unit, amesema haoni kama ni busara kukaa na kuanza kumsema vibaya
kiongozi uliyemchagua mwenyewe ili akuongoze.
“Haya ni matatizo ya club na kuna watu ambao wanahusika kuzungumza
kuhusu udhaifu wa uongozi, siyo kila mtu anaweza akaongea. Tunajua kila
mtu anaweza kuongea lakini nawataka wasanii wenzangu kuwa wastarabu, na
nachukua fursa hii kuwakanya watu ambao hawakupewa ruksa ya kuongea
mambo ya bongo movie. Kwanini uongee bila kuteuliwa uongee? Watu
wanavyoongea wanachochea ugomvi. Tatizo lililokuwepo kwa wasanii
wanataka kila mtu aongee. Hata kama kuna matatizo lazima kuwe na
mazungumzo ya ndani ili kumaliza tofauti zilizopo,”alisema JB.
Katika hatua nyingine JB amezungumzia uwezo alioonesha Q Chillah katika filamu yake mpya ya Hukumu ya Ndoa Yangu.
“Q Chillah kacheza kama kijana Mkenya aliyekuja kuharibu ndoa ya
watu. Q Chillah ana uwezo mkubwa sana kabla Q Chillah hajaanza kuwa
mwanamuziki alikuwa anaigiza katika kundi ambalo lilikuwa linaongozwa na
King Master. Kwahiyo nilikaa na director marehemu Adam akasema huyu
anaweza kucheza hii nafasi na kweli amefanya vizuri sana. Watu waitafute
hiyo filamu waone.”
No comments:
Post a Comment