button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Monday, November 3, 2014

SWALI: ITV Kuendelea Kumpa Airtime Jaji Warioba Sio uchochezi Katiba Mpya Ikataliwe?

Namsikiliza kwa makini sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akiizungumzia mchakato wa kuipigia kura ya maoni, ama kuipitisha katiba pendekezwa au kuikataa.


Kwa vile baadhi ya maoni ya Tume ya Warioba, yalipigwa chini, it is obvious Jaji Warioba, atakuwa ni mpinzani number 1 wa katiba pendekezwa, kwa kupuuza maoni ya wananchi, yaliyopendekezwa na Tume yake.

Kwa vile baada tuu ya kuwasilisha rasmi ile rasimu ya Tume ya Kukusanya Maoni, kwenye Bunge Maalum la Katiba, Tume ya Warioba, ilivunjwa rasmi!, hivyo as of now, Jaji Warioba, sio authority tena katika mchakato huu wa katiba mpya!, bali ni mwananchi tuu wa kawaida, mwenye uhuru wa kutoa maoni yake kama mwananchi mwingine yoyote!.

Jee, kitendo cha ITV kuendelea kumpa airtime Jaji Warioba, huu sio uchochezi wa kupigia chapuo Katiba Pendekezwa, ikataliwe?!.

Anachokifanya Jaji Warioba ni kuwaelimisha Watanzania, kuielewa katiba pendekezwa imekosa nini, hali inayoweza kupelekea katiba mpya kukataliwa!, sasa inachokifanya ITV, ni kuwasaidia Wananchi kuielewa Katiba Pendekezwa, hivyo kuwachagiza kuikataa, jee huu ni ukombozi kwa Watanzania au ni uchochezi?!.

Kwa vile Tume ya Warioba iliisha vunjwa kitambo, kwa nini ITV inaendelea kumkumbatia Jaji Warioba, kwa kumpatia airtime kubwa namna hii, badala ya airtime hii kupatia Andrew Chenge na Samuel Sitta ili wainadi Katiba Mpya?!.

Jee ITV ni wachochezi au wakombozi?!.

Kwa vile mmiliki wa ITV ni Mzee wetu, Mhe. sana, Dr. Reginald Mengi, kama ITV ni Wachochezi, inawezekana pia ikawa mchochezi mkuu ni mzee wetu huyu?!, na ikiwa ITV ni wakombozi, jee inawezekana Mzee wetu huyu ni Mkombozi?!.

No comments: