button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Tuesday, November 18, 2014

Binti wa Kiarabu Aparamia Pombe Amwaga Radhi Hadharani... Mameni Wasisimka

POMBE si chai! Binti mrembo mwenye asili ya Kiarabu ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akifanya
vioja baada ya kulewa chakari na kusababisha midume kumtolea udenda, Ijumaa Wikienda lilimpiga chabo.

Tukio hilo la aibu lilijiri kwenye onesho la Kundi la Mashauzi Classic ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo lilikuwa likitambulisha albam yake mpya ya Sura Surambi, Sura Siyo Roho.

Awali binti huyo alionekana ukumbini humo akiwa mpole na mwenye sura ya soni huku akipata kilaji polepole kabla ya kumkolea na kuwa staa wa kubinuka kihasarahasara na kumwaga ‘lazi’ mbele ya kadamnasi huku akiacha sehemu ya maungo yake nyeti kweupe.


“Jamani pombe mwanaharamu. Muone yule binti wa Kiarabu, kaja mpole lakini hebu ona vituko utadhani kuna skruu imefunguka kichwani,” alisema mmoja wa mashuhuda.Katika hali iliyoonekana kuzidi kuelemewa na kilaji, binti huyo alianza kuwavaa wanamuziki stejini na kuwakumbatia kisha kuinua mguu na kurusha mateke ya kinyumenyume kama mwanasoka, Cristino Ronaldo wa Real Madrid.

Vioja vya binti huyo havikuishia hapo kwani aliwavaa wanaume na kuwakatikia vilivyo.
Wakati tukio hilo likiendelea, jamaa mmoja alimfuata akidai ni mkewe ambapo alimfokea mwanahabari wetu akimtisha kwamba endapo akiziona picha gazetini atamfanya lolote akafie jela Segerea.

No comments: