button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Tuesday, November 18, 2014

Mama Yangu Amenionyesha Baba Yangu Halisi Baada ya Miaka 38, Nimemkataa Laivu

Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi
baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu. 

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?

No comments: