button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Wednesday, October 8, 2014

Milioni 30 za Johari zimepotea baada ya kuzuiliwa kutoka kwa filamu ya ‘Sister Marry’

Muigizaji wa filamu Blandina Chagula aka Johari amesema pamoja na kusikitishwa kutokana na bodi ya filamu nchini kuizua filamu ya ‘Sister Marry’ isitoke, amekula hasara kubwa.
sister_mary_movie
Johari ameiambia Bongo5 kuwa maandalizi ya filamu hiyo yalighalimu
shilingi milioni 30.
“Unajua inauma sana, tumeshindwa kutetea filamu ya ‘Sister Marry’ kutokana na madai eti tumedhalilisha dini. Ina maana hawataki tuzungumzie maisha halisi kwenye filamu zetu? Mimi binafsi imeniumiza sana. Ile filamu imegharimu zaidi ya milioni 30, hebu angalia, Halafu inafungiwa ili isitoke kabisa! Kinachonisikitisha ni kwamba serikali yetu inashindwa kuangalia sisi tunavumbua baadhi ya maovu ya watu ambayo wanayafanya ili kuelimisha jamii. Kwahiyo imefungiwa na kukatazwa isitoke kabisa kwa sababu kuna mambo ya ukweli ambayo tumeyaonyesha. Tumefanya kila njia mpaka sasa hivi tumeshindwa, kwahiyo filamu ya Sister Marry haitatoka tena,” amesema Johari.