button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Wednesday, October 8, 2014

ACHAPWA VIBOKO 120 KWA UUCHAFU, AZIMIA

SHERIA iliyopitishwa na wakazi wa Arumeru mkoani Arusha ya kuwachapa viboko 70 hadi 120 wasichana wanaovaa nusu uchi na wavulana wanaovaa mlegezo, kuvuta bangi, wizi, matusi na ulevi nyakati za kazi imeanza kufanya kazi baada ya kijana Zakayo Leonard (26) kuchapwa viboko 120 kwa makosa mbalimbali likiwemo uchafu wa kutofua nguo zake. 


Kijana Zakayo Leonard (26) akitumikia adhabu ya viboko 120.
Kijana huyo mkazi wa Ilboru, alihukumiwa adhabu hiyo kwa
kuchapwa viboko 70 akidaiwa kutenda  kosa la  kumshambulia baba yake mzazi  aliyetambulika kwa jina la mzee Ng’uraa na kumng’oa jino moja.
Pia alitandikwa viboko 30 kwa kosa la kumtolea maneno machafu mzee wa kimila (Laigwanani) na baadaye alicharazwa viboko 20 kutokana na tabia ya uchafu wa kutofua nguo zake.
Hata hivyo, mara baada ya adhabu hiyo ya viboko 120 kwa mkupuo, kijana huyo alizimia na kushindwa kuinuka wala kutembea hali iliyolazimika kusaidiwa kwa kubebwa na morani wa Kimasai hadi nyumbani kwake.

 
Zoezi la kumsurubu kijana huyo likiendelea.
Adhabu hiyo ilitekelezwa hadharani mbele ya wazee wawili wa ukoo (Laigwanani) waliokuwa wakishuhudia huku mtuhumiwa akitakiwa kutojigusa popote wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo na kwamba iwapo angejishika popote viboko hivyo alivyochapwa vingefutwa na kurejea upya.
Wazee wa makabila ya Wamasi, Waarusha na Wameru wamejiwekea utaratibu wa kimila bila kujali kama unafuata maadili ya mwanadamu kwa kuwaadhibu wahalifu hadharani bila kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.