button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Friday, September 26, 2014

Mwanaume halisi ni yupi? Jamii imetufundisha nini?

Tuko kwenye jamii ambayo tunaambiwa wewe ni mwanaume bila kujua mwanaume ni nani na wajibu wake ni nini. Tumekua na kukuzwa huku tukiiga na kujifunza kusiko rasmi kuwa mwanaume halisi.Kila mtu atakuja na maana ya mwanamme halisi kulingana na tamaduni na alivyoambiwa na jamii anayotoka. Je swali langu la msingi, Mwanaume halisi ni yupi?
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Nilikaa sehemu na kujifunza kitu ambacho labda kinaweza kukusaidia kama mwanaume mwenzangu. Kuna mambo matano ambayo yanafafanua mwanaume halisi kama ifuatavyo;
Mwanaume halisi ni mtu anayechukua hatua
Hii inamaanisha unapokuwa mwanaume lazima jjue kuwa
wewe uchukue hatua za msingi na madhubuti kwa ajili yako, kwa jamii na familia. Usisubiri mtu mwingine achukue hatua fulani wakati wewe upo, ni kitendo cha kujua maamuzi ya msingi na kuyafuata.
Mwanaume halisi huwajibika katika maisha yake
Tuko kipindi ambacho uwajibikaji umekuwa tatizo sana kwetu hivyo kuacha mambo mengi yakiharibika. Jamii imewajibika katika vitu visivyo vya msingi kwa familia zao na kushangaa mambo mbona hayaendi? Kuwajibika kwa ajili ya amani, upendo na familia kwa ujumla. Mwanamme halisi hulisha na kuitimizia familia yake mahitaji ya muhimu kama chakula , makazi, elimu, msimamo wa kiimani na kufundisha maadili yaliyomema kwa familia yake.Mwanamme halisi hutunza watoto aliowazaa na huonyesha upendo kwa watoto hao, haachi watoto wake kila mtaa.

Mwanamme halisi huongoza kwa kujitoa kwa wale anaowaongoza. Uongozi sio kutawala na kufanya kila mtu akuogope na afuate kila unachokiamua, hapana mambo hayako hivyo. Ni uwezo wa kuwadaidia watu wengine namna ambavyo wanatakiwa wawe au waende kwa staili gani kufika kule kunakotakiwa. Kiongozi wa kweli lazima ajitoe kuhakikisha anaowaongoza wanafika wanakohitajika kufika, kwa kutimiza haja zao, kuwapenda na kutokua mbinafsi.
Mwanaume wa kweli anapenda uaminifu. Uaminifu ni kitu ambacho wengi tumepigwa mchanga wa macho na hivyo kudhani ya kuwa uaminfu hauhitajiki kwenye familia zetu au hata kwa wapenzi wetu kwa wale ambao hatujaoa. Kuna mtu mmoja akasema unapokuwa mwaminifu unakuwa na ujasiri wa kusema ninampenda mtu fulani ila usipokuwa mwaminifu hauna ujasiri huo. Je kama wewe ni mwanamme halisi je ni mwaminifu? Najua wengi tumekuwa na stori nyingi na kusema uaminifu hauwezekani ni ndoto tu, lakini kitu kimoja unachotakiwa ujue kama wewe sio mwaminifu kwenye mausiano yako au ndoa yako kuna watu ni waaminifu na ambao familia zao zinaendelea kwa furaha na amani. Wewe ni kuchagua kusuka au kunyoa.
Mwanamme halisi anaacha kumbukumbu nzuri ya kizazi chake. Unachotakiwa kujiuliza je wewe utaacha heshima gani kwa familia yako siku ukiondoka? Au kitu gani kizuri ambacho baba yako alikiacha na ambacho una ujasiri wa kukisema hadharani? Unaweka mpango gani wa kuacha kumbukumbu nzuri juu ya familia yako na wewe mwenyewe?

Hivyo ni baadhi ya vitu nimejifunza sehemu fulani, je jamii zetu tnatambua mwanaume kama nani?