button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Friday, September 26, 2014

Kama unataka kufanya vizuri kwenye biashara, weka mambo yako vizuri



Siku hizi utafutaji masoko umerahisishwa kwa kuwepo mitandao ya kijamii. Lakini wateja wako wanategemea nini kutoka kwako? Inamaanisha bidhaa yako lazima iwe nzuri. Au kwa lugha nyingine upangilie mambo yako vizuri.
beautiful customer service operator woman with headset
Ondoa dhana kwamba ukiwa na bidhaa wateja watakuja tu
Katika ulimwengu wenye ushindani na bidhaa nyingi sana unahitaji kujipanga na kutokuogopa kutafuta masoko kwa kuingia gharama. Ukweli ni kwamba
kama sijakusikia popote au kuona tangazo lako popote siwezi kujua kama upo hivyo basi sikuhitaji. Kwahiyo ni wakati wako wa kuhakikisha unajulikana na unajipanga uonekane sehemu nyingi zaidi kwa huduma na bidhaa ulizonazo.
Usitangaze bidhaa au huduma ambayo hauna
Watu wengi hufanya makosa ya kutangaza kwamba wana bidhaa fulani au wanatoa huduma fulani lakini ukweli ni kwamba hawana hiyo bidhaa wala hawawezi kutoa hiyo huduma. Madhara ya kitu hicho ni kwamba watu wanapoteza imani na wewe na utakapotangaza kitu kingine hata kama unacho hawataamini.
Usibadilishe ubora wa bidhaa au huduma
Biashara zetu nyingi watu huanza kwa ubora wa juu na wateja wanapoanza kuongezeka unaanza kubadilisha na kupunguza viwango ili upate faida kubwa. Kitu unachohitaji ni ujue kwamba bidhaa yako unataka ifike wapi na itambulike vipi ? Ukishindwa kuona mbele, unaandaa kuanguka na kuporomoka vibaya. Ubora wa bidhaa yako au huduma yako ndio biashara yako na si vinginevyo.
Jifunze namna ya kuiongelea biashara yako vizuri

Kitu kingine unachotakiwa kujua ni namna ya kuizungumzia biashara yako mbele za watu au utakapopata mwanya wa kuizungumzia. Watu wengi wanakwama pale wanapotakiwa kusimama mbele za watu na kueleze biashara zao zinashughulika na nini? Wanashindwa kwasababu hawajajiandaa kusimamama mbele za watu na kuongelea biashara zao. Tambua madhumuni ya biashara yako, faida zake, inapatikana wapi au unasambazaje biashara hiyo na watu uliowalenga kuwauzia ni akina nani? Je wakihitaji kukuona au kufika ofisini kwako ni wapi? Je una business card au kipeperushi chenye kuelezea biashara au bidhaa yako n.k!