Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’ ameanza kurejea katika ‘fomu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa
mujibu wa ndugu wa karibu wa msanii huyo , Vengu ambaye kwa muda mrefu
alipoteza kumbukumbu kiasi cha kushindwa kuwatambua watu, sasa amejaliwa
kwani anaweza kuwafahamu watu mbalimbali wanaopata nafasi ya kwenda
kumjulia hali, Kigamboni jijini Dar anakoishi.
“Bado
yupo chini ya uangalizi maalum wa kifamilia, ni watu wachache
wanaruhusiwa kumuona, lakini sasa hivi huwezi kuamini, watu wanaofika
kumtazama anawatambua na anawapa ‘hi’."
Kutokana
na usiri wa hali ya msanii huyo unaofanywa na familia yake, kumekuwa na
maneno chini kwa chini ikiwa ni pamoja na uzushi wa mara kwa mara kuwa,
mchekeshaji huyo maarufu, amefariki dunia na kuzikwa kwa siri jambo
ambalo si la kweli.
Hata
hivyo, katika namna ya kusikitisha, ndugu huyo alisema kuwa kila Vengu
anapomtambua mtu anayemtembelea amekuwa akimwaga machozi hali
inayoonesha kuwa anarejesha nyuma kumbukumbu zake na kugundua amekuwa
mbali naye kwa muda mrefu.
Pia ndugu huyo alisema kwa hali ya Vengu sasa anaweza kurejea kwenye kazi zake za kuchekesha kama zamani zile.
“Kwa jinsi ilivyo, Vengu atarejea hivi karibuni katika kazi yake ya kuburudisha akiwa sambamba na wenzake wa Orijino Komedi kwa sababu afya yake inaimarika sana,” alisema ndugu huyo huku akikataa katakata kutoa ramani ya nyumba anayoishi Vengu.
“Kwa jinsi ilivyo, Vengu atarejea hivi karibuni katika kazi yake ya kuburudisha akiwa sambamba na wenzake wa Orijino Komedi kwa sababu afya yake inaimarika sana,” alisema ndugu huyo huku akikataa katakata kutoa ramani ya nyumba anayoishi Vengu.
Kana
kwamba haitoshi, wakati hali yake ikisemwa na ndugu inaendelea vizuri,
kuna madai kwamba msanii huyo na familia yake wamepewa nyumba ya kisasa
yenye thamani ya shilingi milioni 120, sawa na wasanii wenzake akina
Wakuvanga kufuatia mkataba wa kundi hilo na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF).
“Ni
kweli afya ya Vengu kwa sasa ipo vizuri, anajitambua. Pia amepewa
nyumba, kubwa tu ipo kulekule Kigamboni anakoishi lakini bado
hajahamia.”
Vengu
alianza kuugua kidogokidogo mwaka 2009, lakini Agosti, 2011 hali yake
ilikuwa mbaya, akalazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
jijini Dar. Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kwenda kumjulia hali.
Baada
ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo
nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiaendelea
kuuguzwa na familia yake huku taarifa zake zikiwa ngumu kupatikana mpaka
hivi karibuni ambapo ndugu mmoja aliamua kuweka wazi hali ilivyo kwa
sasa.
Ugonjwa wake mkubwa ulitajwa kushambulia sehemu ya kichwa, hasa kwenye ubongo
No comments:
Post a Comment