button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Wednesday, October 8, 2014

Sijawahi kuwa na uhusiano na Diamond – Meninah

Msanii mrembo wa Bongo Fleva, Meninah amezungumzia kwa mara ya kwanza tetesi za kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz.
meninah
Meninah ameongea na Bongo5 na kueleza ukweli wake kuhusu tetesi hizo.

“Unajua nimekuwa niangalia tu hayo mambo yanavyoenda hasa kwenye magazeti lakini sielewi wao hizo habari wanatoa wapi maana naona wanatengeneza hizo story mara sijui nimevishwa pete! Sijavishwa pete na mtu yeyote yule wala sijawahi kuchat na mtu nikamwambia habari hizo. Naona wanatengeneza sana suala hilo, mie sijui na mahusiano na Diamond,” amesema.
“Kuniathiri kwangu halijaniathiri kwakuwa familia yangu inaelewa ukweli kwamba hamna kitu kama hicho. Kumbuka mie bado naishi nyumbani kwetu na nyumbani wananiamini na wala huyo Diamond hajawahi kunifutalia wala kunitamkia. Yaani huwa namuona tu kwa mbali kwenye matamasha. Na ngoma zangu nilikuwa natamani sana kufanya naye lakini nilikuwa nashindwa hata kumfuta kumwambia sasa hivi mambo hayo yanavyozidi kuendelea ndo kabisa. Halafu unajua Diamond ni msanii mkubwa sana kwahiyo ukitaka kufanya naye kazi lazima ujipange halafu ukizingatia mie bado sio msanii mkubwa kivile ila tokea zamani nilikuwa natamani sana kufanya naye kazi ila kumpata kwake ndo nilishindwa,” ameongeza.
FRONTAMANI
“Ila kiukweli huwa inaniuma sana kuzushiwa vitu ambavyo havina ukweli wowote naona watu wa magazeti ndo wanalazimisha iwe ivyo kwakuwa wanaona kila msichana mrembo lazima awe na Diamond. Sio sawa kuandika vitu ambavyo sio vya kweli halafu hawana vithibitisho maana siku ya siku hata mtu alikuwa hana mpango na wewe lakini ataona ‘mbona wananiandika sana kuhusu huyu Meninah’ yule mwanaume unajua ndo watamfanya sasa aanze kunifuatilia, maana Diamond ana mpenzi wake kila mtu anamfahamu Wema. Na kuhusu sijui Wema kunitumia watu hamna kitu kama hicho, sijawahi kutumiwa mtu yeyote yule kwahiyo napenda watu waelewe hivyo.”
Kwa upande mwingine muimbaji huyo amesema anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Kaniganda’.