Msanii wa filamu Rose Ndauka ambaye alikuwa mbioni kufunga ndoa na mzazi mwenzake, msanii wa kundi la TNG, Malick Bandawe maarufu kama King Chiwaman wameachana kutokana na kutoelewana ndani ya mahusiano yao.
Rose Ndauka na Chiwaman
Akizungumza na bongo5 leo, Rose amesema wamejaribu kukaa chini na kuyaweka sawa mahusiano yao lakini imeshindika na kuona sulihisho ni kuachana.
“Ni kweli tumeachana hivi karibuni. Kuna sababu ambazo zimetufanya mahusiano yetu yaishie hapo. Tumekaa chini na kuzungumza lakini hicho ndicho tumeona ni kitu cha kufanya na cha busara,” amesema Rose.
Kwa upande wake Chiwaman alipost picha ya mtoto wao Instagram huku akiwa ameandika ujumbe wa kuumiza.
“Pain makes you stronger, fear makes you braver.Heartbreak makes you wiser…..I will miss you my naveen and its painful that you will have to call another man FATHER….a wonderful gift, may you take good care of your family and i will always love you my Naveen.”