ay Z na Beyoncé wanaingia studio kurekodi album mpya ya siri pamoja.
Wawili hao ambao walimaliza ziara ya pamoja ‘On The Run’ jijini Paris mwezi uliopita, wanarekodi kwa siri pamoja na
wanapanga kutoa album ya surprise mapema mwaka huu ama mwanzoni mwa mwaka ujao, kwa mujibu wa mtandao wa Page Six.
Wanandoa hao wana matumaini ya kurudia mafanikio ya album ya Beyonce iliyotoka December mwaka jana na kufanikiwa licha ya kutofanyiwa promotion yoyote. Utoaji huo wa album usio wa kawaida umepelekea kufanyika kwa utafiti kwenye chuo kikuu cha biashara cha Havard.
Inaaminika kuwa wanandoa hao maarufu watasindikiza uzinduzi wa album hiyo na video kadhaa pamoja na filamu.