button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Friday, September 19, 2014

SIKIA UPUUZI WA WADADA WA BONGO MOVIES!

NENO la Mungu linasema siku za mwisho maovu yataongezeka, ni kweli maandiko hayo yameanza kutimia duniani. Leo nazungumza nanyi baadhi ya waigizaji wa kike katika tasnia ya filamu za nyumbani ambao mmekuwa na tabia ya kunyang’anyana wanaume. Ndiyo, mnajijua.
Wolper.
Hadi nafikia hatua hii ya kuwaandikia makala haya nimelalamikiwa na watu kibao kuhusu tabia yenu hiyo ya kuzungukana kwa wanaume zenu jambo ambalo limesababisha chuki kati ya mtu na mtu huku wengine mkifikia hatua ya kurogana.
Tabia hii siyo nzuri kwani wanaume wapo wengi sana, kwanza ninyi ni wasichana warembo, wazuri na mna kila sifa ya kumvutia mwanaume yeyote aliyekamilika. Kwa nini msitulie na kujiheshimu msubiri wa kwenu ambaye Mungu amewapangia kuliko kunyang’anyana?
uwoya
Utakuta mtu una mpenzi ndani ya tasnia na baadhi ya wasanii wenzako wanajua lakini kinachoshangaza ni pale ambapo anatokea rafiki yako wa karibu na kukupindua angali mlikuwa mnaitana wifi.
Hii inaumiza, inakera na inachafua sifa nzima ya tasnia kwa sababu jamii inataka kujifunza mengi kutoka kwenu, sasa mnataka ijifunze huo ufuska wenu? Hiyo haiwezekani kwa sababu kutakuwa na kizazi cha uovu kitakachoongeza maasi duniani.
Baadhi yenu siku hizi mkishapata wachumba mnaogopa hata kuwatambulisha kwa rafiki zenu kwa kuhofia kuibiwa jambo ambalo ni hatari kwani mnakoseana imani wenyewe kwa wenyewe yaani mnajitesa mioyo yenu kwa mambo ya kipuuzi.
Niwape mfano; hivi karibuni wewe msanii chipukizi wa filamu, Brenda Marembeka ‘Kunguru’ ulimeza vidonge kwa lengo la kuutoa uhai lakini ukaokolewa na hii ni baada ya kutokea kwa mzozo wa kimapenzi mkimgombea mwanamuziki wa Kundi la Makomando, Muky ambaye kwa tetesi zilizozagaa mitaani alikuwa akigombewa na wasichana watatu wa Bongo Movies.
Baada ya kutokea mzozo huo habari zinasema kuwa kwa sasa mwanamuziki huyo yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja (jina kapuni) wa Bongo Movies ambaye ndiye aliyekutukana ukaona bora ufe kuliko kumkosa msanii huyo.
Mnakumbuka sakata la Jacqueline Wolper na Irene Uwoya? Leo ni chui na paka kisa ni huyo Ababuu aliyekuwa mchumba wa Wolper akadaiwa kunyakuliwa na Uwoya. Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ unajua kilichotokea kati yako na Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ mliponyang’anyana mwanaume?
Ukweli tabia hiyo inakera sana, wasanii wa kike badilikeni kwani mnatia aibu. Tulieni kwani wanaume wako wengi kwa nini mnang’ang’ania kwa mwanaume mmoja tambueni kwamba kuna ugonjwa hatari wa Ukimwi kama mmoja anao itakuwa rahisi sana kuwaambukiza wengine. For the love of game!

No comments: