button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Sunday, September 11, 2016

Fao la kujitoa NSSF, PSPF, GEPF Laleta Utata kwa Wanachama.


WAKATI serikali ikijipanga kuwasilisha bungeni muswada wa sheria kuwabana wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kujitoa, vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia vimepinga na
vimetoa msimamo mkali.
Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu fao la kujitoa (kushoto) Rais wa TUCTA na CWT, Gratian Mukoba (kulia) katibu wa chama cha wachimbaji madini nicomemas kajungu.
Serikali inatarajia kuwasilisha kwa hati ya dharura muswada huo bungeni unaokusudia kuzuia fao la kujitoa kwa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii,
Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Chama cha Taasisi za Elimu ya Juu, Habari na Utafiti (Raawu), Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (Tuico), Chama cha Wafanyakazi wa Hoteli na Nyumbani (Chodawu), Chama cha Wafanyakazi wa Madini na Nishati (Numet) na mitandao ya asasi za Kiraia Tanzania chini ya mwavuli wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Tamko hilo limetolewa baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamiii kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inaandaa muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambao kwa sasa uko katika hatua za mwisho, huku ikielezwa kuondolewa kwa fao la kujitoa na badala yake kuletwa fao la kutokuwa na ajira.
Akisoma tamko hilo jana jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari, Rais wa TUCTA na CWT, Gratian Mukoba, alisema mchakato wa kubadilisha sheria za mafao ulipaswa kuwa shirikishi kwa kuwahusisha wenye mifuko hiyo na wafanyakazi kupitia vyama vyao vinavyotambulika kisheria.
“Jambo linaloshangaza ni usiri mkubwa uliopo katika jambo hasa lengo la kutaka kupeleka mswaada huu kwa hati ya dharura bungeni bila kutoa ushiriki wa wadau kikamilifu,” alisema Mukoba.
Alisema kuwa fao la kujitoa lina madhara hasa kwa wale ambao wataacha kazi, kwa sababu lengo la mifuko hiyo ni kumtunza mtu baadaye atakapopoteza uwezo wa kufanya kazi.
“Kijana anaanza kufanya kazi akiwa na miaka 20, unakuja kumwambia akitimiza miaka 60 ndipo unamlipa mafao yake baada ya kuacha kazi kwa maana hiyo unamthamni akiwa kijana akiwa mzee humthamini,” alisema Mukoba.
Aliongeza kuwa serikali inapaswa kuwashirikisha wadau wote katika kutunga sheria na masuala mengine ya kazi na fao la kujitoa libaki kuwa haki kwa wafanyakazi wa ajira za muda na zisizozidi miaka 15.
“Fao la kujitoa ni takwa la mikataba ya ILO (Shirika la Kazi Duniani), hivyo lilitolewa na bila vikwazo na serikali ilisimamie hili. Fao hili lisiishie kwa wale waliopoteza ajira tu, bali kama linavyoitwa fao la kutokuwa na ajira na lipelekwa kwa Watanzania wote wenye sifa na haki ya kuajiriwa,” alisema.
Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, alisema wanafunzi wengi wanapomaliza elimu zao za vyuo wanapenda kufanya kazi kwa muda ili baadae watumie fao la kujitoa kujiendeleza kielimu, hivyo kusubiri mpaka wafikishe miaka 60 ni sawa na kumnyima haki yake ya kupata elimu.
“Watu wengi wanapoacha kazi au mikataba yao inaopokuwa imekwisha katika maeneo ya kazi hupenda kufungua biashara binafsi badala ya kuajiriwa upya na mtaji wanaotegemea ni fao la kujitoa,”alisema Olengurumwa.
Aliongeza kuwa ni vigumu kuingia akilini kuwa Tanzania imefikia hatua ya kutaka mtu aache kazi akiwa na miaka 25 au 30, akae hadi afikishe miaka 60 ndipo achukue pesa zake sawa na yule anayefanya kazi hadi kustafu.
Aliongeza kuwa uelewa wa matumizi ya pensheni umekosekana kwa kuwa lengo la fao ni kumsaidia aliyekoma kufanya kazi maisha yake yaendelee kama alivyokuwa kazini na si kumfikisha miaka ya kustaafu.
Olengurumwa alisema wanawasihi wabunge kama waathirika wa mabadiliko ya fao la kujitoa, kusitisha majadiliano ya muswada huo unaotarajiwa kusomwa mara ya kwanza kwenye vikao vinavyoendelea, hadi serikali irejeshe kipengele cha fao la kijitoa.

No comments: