TUKUBALI tukatae, sakata la fedha kiasi cha Sh. bilioni 306 zilizochotwa kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limeipasua nchi, Risasi Jumamosi limegundua.
Escrow imeipasua nchi kufuatia majadiliano ya waheshimiwa wengi kuanzia juzi, Alhamisi kuonekana kila mmoja ana upande wake huku wapiga kura wao nao wakiwa kinyume na wawakilishi hao.Risasi Jumamosi liligundua kuwa, mara tu baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kujitetea kufuatia uchunguzi wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kumtia hatiani kuhusika na uchotwaji wa fedha hizo, mitandao ya kijamii ilianza kugawanyika.
Mitandao hiyo, tofauti na ilivyokuwa kabla ya Waziri Muhongo hajajitetea ambapo ilikuwa ikisisitiza aachie ngazi, ilianza kumtetea na kusema Kamati ya Zitto iliumbuka ikidai mheshmiwa huyo alijitetea vizuri kwa kuanika ukweli wenye ushahidi.
Katika uchangiaji wa hoja kwenye mitandao, wengine waliwapinga wanaomtetea Muhongo wakidai walipewa ‘kitu kidogo’.
Hata hivyo, katika mjadala wa bunge hilo jioni ya juzi, mchangiaji wa kwanza, mheshimiwa Tundu Lissu alipopewa nafasi na kupingana na utetezi wa Profesa Muhongo, mitandao ya kijamii nayo ikagawanyika tena ambapo wengi walisema Lissu alikuwa na hoja.

No comments:
Post a Comment