Muigizaji wa filamu nchini Kajala Masanja anatarajia kuja na filamu mpya iitwayo Tishu ambayo itasambazwa na kampuni yake mwenyewe.
“Sasa hivi ni mwendo wa kazi tu, sasa hivi tupo kwenye maandaliazi ya filamu yangu mpya ya Tishu, ni filamu ya comedy na Tishu ni jina la mtu aliyeigiza humo ndani ya filamu,” Kajala aliiambia Bongo5.
“Hii filamu kusema ukweli tutaisambaza wenyewe chini ya kampuni yangu, watu wakae mkao wa kula na ile short film ya ‘Mbwa Mwitu’ itaanza kuoneshwa soon kwenye TV.”