Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Mbeya walipotembelea Ofisi za ubalozi Nchini Malawi
Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi
Baadhi ya Waandishi wa Habari Kutoka Mkoani Mbeya wakimsikiliza Balozi kwa Makini
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akipokea Taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akijibu Taarifa ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya .
Waziri wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa akiongea na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Mh. Kondwani Nankumwa
Wa kwanza Kulia ni Afisa Habari wa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni akifuatilia Mkutano huo
Waandishi wa Habari wakiendelea kufuatilia Kikao hicho
Francis Phiri wa kwanza Kulia ambaye ni Mratibu wa ziara hiyo Nchini Malawi na Muasisi wa Nyika Press Club ya Malawi akiwa katika Mkutano huo.
Kikao kikiwa Kinaendelea
Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Kutoka Mkoa wa Mbeya nje ya Ofisi yake Jijini Lilongwe.
Waziri wa Habari,Utalii na Utamaduni nchini Malawi Mheshimiwa Kondwani Nankhumwa alisema kuwa Serikali ya Malawi haina mgogoro na Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.
Aliyasema hayo baada ya kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa Mkoa wa Mbeya waliotembelea ofisini kwake katika mfululizo wa ziara ya waandishi waliofanya ziara ya juma moja nchini humo katika ziara ya kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa Nchi hizo.
Waziri Nankhumwa alisema kuwa Mtoto wa Rais wa Malawi Profesa Ather Muthalikana anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa Muhadhiri wa chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi na kufanya biashara nchini Malawi hivyo hakuna sababu za kuwepo kwa tofauti za aina yoyote ile itayowapelekea kuwagawa wananchi wa pande hizo.
Aidha alisema kuwa ili kuonesha hakuna tofauti baina ya wananchi wa pande hizo Marais wa nchi hizo watapaswa kuchukua ndoano na kuvua samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia kuwa wananchi wa pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa makabila.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere ambaye alisema kuwa hakuna mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.
Aliyasema hayo alipotembelewa na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi katika mfulizo wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi ili kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali zikiwemo za mazingira,utalii na Elimu juu ya Ukimwi ambazo zinafanana katika nchi hizo.
Balozi Tsere alisema hivi sasa si wakati wa marumbano kwani inahitajika subira katika mzungumzo yaliyonza baina ya viongozi wa nchi hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo katika mahakama ya kimataifa ambapo utazigharimu fedha nyingi nchi hizo katika utatuzi wa mgogro huo.
Hata hivyo Waandi wa Habari wa nchi hizo walifanya makubaliano ambayo yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama zilizopo Malawi na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili utumiwe na wananchi hizo ili kukuza uchumi wan chi hizo.
Katika ziara hiyo Waandishi wa vyombo mbalimbali walishiriki ikiwa ni pamoja na Tone Multimedia Group, Mbeya yetu Blog,Chanel Ten,Mwananchi,Jambo leo,Bomba Fm,Majira na Raia Mwema.
Vingine na Tanzania Daima,Baraka FM na Mwandishi Rais mstaafu Ulimboka Mwakilili ambaye alikuwa Mwenyekiti wa safari na Mhandisi wa Ujenzi Claudio Lusimbi ambaye ni Mlezi Katika Safari hiyo
No comments:
Post a Comment