TID anasema anammiss kupita kiasi swahiba wake, marehemu Albert Mangwea aka Ngwair.
TID ameiambia Bongo5 kuwa Ngwair alikuwa na msaada mkubwa kwenye muziki wake.
“Unajua kukosekana kwa Ngwair kwangu ni pengo ambalo siwezi kulisahau
kabisa,” amesema muimbaji huyo. “Unajua ua Ngwair kuna ngoma tulikuwa
tunafanya wote na msaada wake nilikuwa nauhitaji sana maana touch zake
zilikuwa nzito. Kama nyimbo zangu ‘Kiuno’,’Raha’,’Check Me’, zote hizo
ameandika yeye Ngwair. Ukiacha hizo tulikuwa tunataka kuja na kipindi
cha TV, kufanya movie ya Girlfriend Part 2. Vitu vyote hivyo ni mtu
ambaye tulikuwa tumeanza naye. Leo unaona hayupo najiona nipo mpweke
sana, maana ni mtu ambaye alikuwa akinipa idea, aisee nammiss sana,”
ameongeza TID.
Kwa upande mwingine TID amezungumzia uhusiano wake na Dully kutokana na taarifa za hivi karibuni kuwa walizinguana.
“Mimi na Dully hatuna tofauti tu ni chalenji tu na juzi Dully
alikuja home tuakenda studio tumerekodi ngoma ya pamoja. Kwahiyo sisi
tunafanya chalenji ili tufanye kitu kizuri. Dully ni kama brother wangu
amenipita mimi kama mwaka mmoja na mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanza
kumtambulisha Dully stejin pale Bills enzi hizo miye nilikuwa MC wa
hapo.”