Kajala Masanja amedai kuwa maisha yake hayajabadilika sana kama ambavyo magazeti ya udaku yamekuwa yakiandika.
Muigizaji huyo wa filamu alisema kuwa tetesi kuwa ana fedha nyingi
kiasi cha kuwa na mpango wa kumwajiri Wema Sepetu ni uzushi mtupu.
“Mbona maisha yangu ni ya kawaida sana,” Kajala aliiambia Bongo5.
“Mimi naona nipo vilevile hakuna kubwa sana lililongezeka. Nafanya
shughuli zangu tu. Tatizo watu wanaamini sana magazeti. Mimi i sina
utajiri huo wanaouzungumzia, Kajala ni yule yule,” alisisitiza.
Hivi karibuni Kajala alizindua filamu yake fupi iitwayo ‘Mbwa Mwitu’.