button

anim

Tally

advert2

security

Advert

Advert
Advert

babu

babu
leokwetu

mochrispoadver

pub

pub

flashplayer

Monday, November 24, 2014

Watanzania Tumekwisha! Eti India na Kenya Zaongoza kwa Uuzaji Madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania Pekee!

Taarifa kwamba nchi za Kenya na India zimeipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha madini ya Tanzanite yanayopatikana hapa nchini pekee na kuyauza katika soko la dunia ni jambo ambalo siyo rahisi kuliamini.

Nasema siyo rahisi kuamini kwa sababu haingii akilini hata kidogo, mtu ambaye

halimi mahindi anaibuka kinara wa kuuza sokoni mahindi yako anayoyaiba shambani kwako.

Ni heri kama angekuwa anakuja kununua kwa njia ya kawaida na wewe ukanufaika.

Nilimsoma kwa makini Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja hivi karibuni kupitia baadhi ya magazeti nchini akisema kwamba kwa mwaka jana, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Mwaka jana pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 100 milioni (Sh173 bilioni), dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni), zilizouzwa na Tanzania.

Katika kipindi hicho cha mwaka jana, India iliuza Tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola 300 milioni za Marekani(Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India.

Mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka Marekani, aliwahi kuwauliza viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini iwapo kuna migodi ya Tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata Tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.

Taarifa zinaeleza kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya Tanzanite inayopatikana Mirerani, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, huuzwa kwa njia za panya nje ya nchi na kwamba Serikali imeanza kuchukua hatua.

Kama nilivyosema awali, hili ni jambo la kushangaza sana. Ninajiuliza; hivi haya madini nani anayeyatorosha kwenda nchi za nje? Ni wazi kuwa watu wachache waliopewa jukumu la kusimamia sekta ya madini, wamekuwa wakishirikiana na watu wa nje kutorosha madini hayo.

Tumejua wizi wa madini haya kwa sababu tu yanapatikana pekee Tanzania. Tujiulize wizi huu wa madini yetu ukoje katika madini mengine ambayo pia yanapatikana katika nchi nyingine?

Kwa hakika, raslimali za nchi hii zinaliwa na watu wengine, huku Watanzania wakibaki mikono mitupu.

No comments: